Header Ads Widget

RUKSA KUTANGAZA NIA, ILA MARUFUKU KUSEMANA VIBAYA – CCM IRINGA


mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wa Iringa Daud Yassin (katikati)akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kulia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa (MCC) Salim Faraj Abri na kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Iringa Said Goha picha na Matukio Daima Media.

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa kimepiga marufuku wanachama wa chama hicho wanaotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwachafua wagombea wengine kwani si jambo la hekima na busara. 

 Hayo yamesemwa na Mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa Salim Abir Asas wakati akizungumza na wanahabari mkoani hapo na kueleza kuwa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu na ndani ya chama kuna michakato mingi ya uchaguzi ambayo lazima ifuate utaratibu.


 Alisema kuwa kwa sasa Chama hicho kinapitia mchakato wa ndani ya chama wa kura za maoni,huku baadhi ya watia nia tayari wameanza kutangaza nia zao. " Tunawasihi na kuwashauri wale wanaotia nia kwamba kama wanaitisha waandishi wa habari kuelezea nia zao basi waelezee kwanini wametaka kugombea bila kutoa shutuma yeyote" TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

 " Wewe umekuja unaomba nafasi sio busara kumchafua mtu mwingine kwa sababu watakao amua ni wapiga kura hivyo nawasihi sio busara kumshutumu mtu kwa sababu wote wanatokea ndani ya chama"

 Aidha Asas aliwataka wanahabari watakapokuwa wanapokea habari ambazo zinaweza kumkwaza mtu ama chama ni vyema kubalance habari hizo badala ya kutoa taarifa za upande mmoja. 

 " Ninyi kama wana habari ni vyema mkathibitisha tuhuma zinazotolewa baina ya wagombea kama ambavyo taaluma yenu inawakata kwa sababu wagombea wote ni wa CCM" alisema Asas 

 Aliongeza kuwa wao kama chama wametoa angalizo hilo kama tahadhali katika Mkoa wa Iringa,kwa sababu chama kina kanuni uteuzi wa wagombea wa uongozi katika vyombo vya dola amnayo inatumika katika nchi nzima. 


 Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin amempongeza Salim Asas kwa kupata nafasi hiyo ya MCC na kuwa mkoa umepata heshima. 

 " kwenye chama chetu mjumbe wa kamati kuu ya taifa sio jambo dogo,tumeipokea nafasi hiyo kwa furaha na kwa shukrani kubwa kwa Dkt Samia Suluhu Hassan"alisema Yassin 


Alisema kuwa wagombea wanaotangaza kugombea nafasi mbalimbali kupitia CCM wanapaswa kujitafakari kwa kina namna watakavyowasilisha hoja zao kwa wapiga kura badala ya kutoleana maneno machafu. 

Hadi sasa Chama cha Mapinduzi tayari mgombea wa nafasi ya Urais ni Dkt Samia Suluhu Hassan nafasi zinazogombewa ni ubunge na udiwani pekee.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI