Header Ads Widget

RAIS DKT. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI WA MABADILIKO YA TABIANCHI SIMIYU.



Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi unatekelezwa Mkoani kwa gharama ya shilingi Bil. 440.


Akizungumza kwenye Mradi huo, Rais Dkt. Samia amesema kuwa katika mikoa inayozunguka Ziwa Victoria imefikiwa na huduma ya Maji na kwmaba serikali inakamilisha miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa ili kufikisha huduma za Maji.


Amesema kuwa jitihada hizo zimeimarisha upatikanaji wa Maji safi na salama katika Mkoa wa Simiyu, kutoka wastani wa asilimia 70 mwaka 2020 hadi asilimia 83 mwaka 2025.


Ameitaka Wizara ya Maji, kushirikia na viongozi wa Mikoa na wilaya ili kuimarisha Utekelezaji wa Mipango ya Upatikanaji wa Maji safi na salama.



Amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutoa ushirikiano wakati wa Utekelezaji wa Mradi huo ambao utakuwa mkombozi kwa wananchi wa Mji wa Lamadi, Nyashimo, Bariado, Langangabiili pamoja na vijiji 103 katika awamu ya kwanza.


"Nimetaarifiwa baadhi yenu mmejitolea maeneo bure ili kutekeleza Mradi huu ambao mmechangia Utekelezaji wa Mradi huu, hongereni kwa uzalendo...tunapoenda kuendelea na Utekelezaji wa awamu ya pilo Meatu na Maswa tutor ushirikiano ili kuharakisha Utekelezaji wa Mradi huu" amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI