Na Shemsa Mussa -Matukio daima
Kagera.
Ongezeka la bei ya kahawa limekuwa tishio kwa wakulima huku wezi wakiiona kama fulsa kuvamia mashambani na kuvuna zao Hilo.
Akizungumzia suala Hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg Isaya Mbenje wakati alipotembelewa na Mwandishi Wetu ofisini kwake, amesema baada ya ongezeko la bei ya zao la kahawa imetokea changamoto ikiwemo wezi kulishambulia zao Hilo pamoja na wakulima kuvuna kahawa zikiwa mbichi (Butula).
Amesema kutokana na changamoto hizo wameanzisha ulinzi shirikishi Kila kitongoji kupitia Serikali za vijiji,ikiwa Kila kitongoji kuhakikisha Kila ifikapo Saa mbili usiku ndani ya kitongoji asiwepo mtu anayezurula bila sababu za Msingi,pamoja na adhabu Kali kutolewa dhidi ya atakayebainika kushiriki uharifu huo.
Aidha amesema katika Halmashauri hiyo wamepiga marufuku ya ununuzi horela wa zao Hilo kwenye Kila Kijiji,ikiwa upo utaratibu wa kahawa zote kukusanywa kwenye vyama vya Msingi na kuuzwa kupitia mnada ikiwa ni utaratibu na maelekezo kutoka bodi ya kahawa na Serikali kwa ujumla.
"Mtu yeyote atakayeonekana kijijini ananunua kahawa kwa maana hiyo atakuwa amevunja sheria na utaratibu wa nchi na anatakiwa kuchukuliwa hatua kali ,kahawa inanunuliwa kwenye chama Cha Msingi na ikitoka hapo inapelekwa kwenye mnada na inauzwa na wanunuzi walio sajiliwa kupitia bodi ya kahawa nchini,amesema Bw Mbenje"
Pia Bw Mbenje amesema kumekuwepo na utamaduni wa baadhi ya wakulima kuuza kahawa mbichi ambayo haijakomaa maarufu kama (Butula) amesema imekuwa changamoto huku akisema wanaendelea kutoa Elimu kwa wakulima ili wajue madhara yake na kuwahamasisha kuwa na mazao mbadala ambayo yanaweza kuwaingizia kipato ili kuhakikisha wanaiacha kawaha inakoma na wafahidike na bei nzuri ya sokoni.
"Ukiuza kahawa ikiwa Butula maana yake unapoteza ile thamani kubwa ambayo ungeipata wakati wa msimu kwa hiyo tunaendelea kutoa Elimu kupitia vyama vya ushirika lakini pia kupitia vyama vya Msingi na tumeanza kuwa na utaratibu wa kutoa Malipo ya awali kwa wakulima na vyama vingi vinafanya hivyo kuhakikisha Yale mahitaji ya Msingi ya mkulima anayapata wakati akisubilia kahawa zake zikomae Shambani,ameongeza Bw Mbenje "
Hata hivyo amekemea tabia ya baadhi ya wakulima katika vijiji kuanika kahawa chini ikiwa Hali hiyo inapunguza ubora wa zao Hilo na katika Hilo wanaendelea kuwatumia maafisa ugani,watendaji na viongozi wa wananchi kuwahimiza kutafuta matandazo na sehemu nzuri ili kahawa ikienda sokoni iendelee kuwa na ubora ule unatakiwa.
Amewasisitiza wakulima wa zao Hilo la kahawa kutorubuniwa na mtu yeyote kwa kuuza kahawa kwenye bakuli, ndoo au beseni ikiwa akifanya hivyo atapoteza fedha ambazo atajuta baadae huku akisema bei ya zoa Hilo inaongezeka Kila siku.
0 Comments