Header Ads Widget

NGAJILO AJITOSA UBUNGE IRINGA MJINI.

 


NA MATUKIO DAIMA APP.

IRINGA.Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo ametangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini Kuelekea katika uchaguzi Mkuu.

Ngajilo ameonyesha dhamira yake ya kulitaka Jimbo la Iringa Mjini mara baada ya kujitokeza katika Ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Mjini Leo kuchukua Fomu ya Ubunge na kuongeza kuwa nia anayo na ana utayari wa kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo.

Amesema kuwa Chama kikimpa Nafasi ya kuwa Mgombea atahakikisha anapigania Maslahi ya wananchi wa Jimbo la Iringa Kwani amekuwa mzoefu katika Nafasi mbalimbali za Uongozi na katika Chama Cha CCM.

alieleza kuwa zoezi la kuchukua fomu kwake ni kwa mara ya tatu, ambapo mwaka 2010 aliomba nafasi ya Ubunge Iringa mjini lakini kura hazikutosha, 2020 aliomba pia na mwaka huu 2025 

"Ninawaahidi chama cha mapinduzi na wanachama wote tutashirikiana vizuri kukijenga Chama na kuhakikisha kinazidi kukubalika kwa sababu kadri watenda kazi wanavyofanya kazi vizuri ndio chama kinazidi kukubalika"alisema 

aliongeza kuwa" Niwaahidi wananchi wa Iringa mjini kwamba tutashirikiana kuhakikisha tunaleta mabadiliko na kuleta maendeleo katika sekta Zote za kimaendeleo, ndani ya manispaa na jimbo la Iringa"

Alisema kuwa kwa sasa wamechukua fomu kuomba ubunge na kusubiri kuitwa na vikao vya chama na kujieleza pale watakapotakiwa. 

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI