Header Ads Widget

PETER MSIGWA ATIA NIA IRINGA MJINI.

 

NA MATUKIO DAIMA AAP.

IRINGA.Kada wa Chama Cha Mapinduzi Mchungaji Peter Msigwa ameeleza kuwa CCM ndio ina viongozi bora,wataalamu, rasilimali watu na fedha pamoja na sera za kuondosha umaskini kwa watanzania.

Msingwa amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la iringa mjini na kueleza kuwa kwa sasa hakuna chama chochote cha siasa chenye rasilimali watu na fedha na sera  ambazo niza kuwakwamua watanzania kutoka kwenye umasikini.

alisema kuwa lengo la kuchukua fomu ni pamoja na kuungana na watanzania wengine katika kuuchukia umasikini na kuuondoa umasikini ambao Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuondosha umasikini.


"Na mimi wananchi wa Manispaa ya Iringa wakinipa ridhaa nitahakikisha nakuwa kiunganishi kati ya wananchi na serikali, kuwa sauti ya wanyonge, na kuwajibika kwa dhamira yangu,kuwajibika kwa wapiga kura wangu na kuwa mzalendo na nitahakikisha tunaendelea kusaidiana na CCM kuondoa umasikini na kuwafanya wananchi kujua haki zao"

Alisema amechukua fomu kama takwa la kikatiba, na kuwa na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi wa Iringa mjini, ambayo wanahitaji sauti kubwa,weredi na kuwa ni mji wa kihistoria unahitaji saiuti pana kuhakikisha mji unaendelea kuwa kwenye ramani.

Msigwa aliwahi kuwa Mbunge takribani miaka kumi akiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na baadae mapema mwaka huu kuamua kuhamia chama cha Mapinduzi na kuendana na sera ya chama hicho.

Zoezi la uchukuaji fomu  za kuwania nafani mbali mbali ikiwemo ya ubunge na udiwani kwa watiania wa chama cha mapinduzi (CCM) limeanza rasmi  leo june 28,2025, huku Mchungaji Msigwa akijitokeza wanza kuchukua fomu.

Akimkabidhi fomu hiyo ya ubunge baada ya kuilipia kiasi cha Tsh 500,000 katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Hassan Makoba alisema wajibu wa kila mtia nia kwenda kujaza fomu na kurejesha pia anatakiwa kuheshimu kanuni za CCM na kuepuka kuanza kampeni kabla ya muda pamoja na kungatia makatazo mengine yote.

"Kuchukua fomu sio kwamba umefunguliwa dirisha la kufanya kampeni hiyo ni marufuku kwa mujibu wa kanuni,pili ni kutoa takrima, fedha au vitu kwa wajumbe pia ni kinyumbe na sheria na kikubwa ni kutoa rushwa kwa sababu nia adui wa haki na nikosa la kimaadili utakuwa umepoteza sifa ya kupendekezwa kuwa mgombea"alisema 

Makoba alisema zoezi hilo limeanza na kuwa mwanachama wa kwanza kupewa fomu hiyo ni Peter Msigwa ambae amefika mapema zaidi na kutoa wito kwa wanacha wengine kuendelea kujitokeza.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI