Lindi Ikiwa ni siku ya pili ya maonesho ya madini Mkoani Lindi yakiendelea Katika viwanja vya Madini huko Wilayani Ruangwa Leo yametanguliwa na Mbio za riadha kwa ajili ya uwekezaji iliyobeba kauli mbiu ya "mbio za riadha uwekezaji kimbilia FURSA Lindi " zikiwa na lengo la kuhamadisha uwekezaji.
Mbio hizo zimefanyika Leo juni 12 zilihusisha viongozi mbalimbali, wananchi pamoja na wadau wa Madini zikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi.Zainab telack ambapo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Jamii kujenga mazoea ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwa mara ili kuimarisha Afya zao.
"Afya bora ndiyo msingi wa maisha na maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Tunapaswa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kila wakati ili kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali," alisema RC Telack.
Aidha, alihamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujifunza kupitia maonyesho ya madini, ambayo yameleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kielimu kwa wakazi wa mkoa wa Lindi na maeneo jirani.
Maonyesho hayo yanalenga kuhamasisha maendeleo ya sekta ya madini na kutoa nafasi kwa vijana kujifunza teknolojia, usindikaji, na fursa za uwekezaji zilizopo katika rasilimali za madini.
0 Comments