Header Ads Widget

KIKWETE: PPRA TUMIENI WANASIASA KUTANGAZA ASILIMIA 30 ZA MAKUNDI MAALUM.

 

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi  vijana, ajira na wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete  ameitaka mamlaka ya ununuzi wa umma (PPRA) kuwatumia wanasiasa katika kutoa elimu na kutanga fursa ya asilimia 30 za zabuni za ununuzi kwa makundi maalum ya vijana na wenye ulemavu.

Kikwete ameyasema hayo wakati akihutubia katika kongamano la 9 la mamlaka ya ununuzi wa umma  linaloendelea mkoani  Arusha ambapo alisema kuwa  changamoto kubwa iliyopo ni mapungufu ya kimfumo ambapo taarifa hazifiki kwa wakati kwa wahusika.

Ameeleza kuwa kwa kutumia kundi la wanasiasa ambao kwao kwa kutangaza fursa hizo ni sehemu ya kuonekana  katika jamii, wanavyoijali na kuitambua ambapo alishauri katika vikao vijavyo wahakikishe wanawakaribisha wakurugenzi ambao ni watendaji, wenyeviti wa halmashauri na mameya wa majiji ili waje kupata elimu ili wajue ni jinsi gani watakavyoenda kuzisimamia hizi asilimia 30

Amesema elimu zaidi inatakiwa  kutolewa kwa wadau ili waweze kuzikimbilia fursa hizo ambao wanapokuwa wanatenga asilimia 30 ni mihimu kwao kuzingatia kuwa watu ambao wanatakiwa kufikiwa na fursa hizo  hawana uelewa wa kutosha hivyo ni jukumu lao wao ambao ni wadau katika utekelezaji wa sheria hiyo kuhakikisha kwamba wana waelewesha na kuwaambia nini wanachotakiwa kufanya.


"Wengi wanafahamu zaidi upatikanaji wa asilimia 10 kuliko asilimia 30 hizi za manunuzi ya umma  kwa hiyo ninasisitiza juu ya umuhimu wa utoaji wa elimu, sijui mnanielewa? kwamba watu wanaotakiwa wapelekewe hizi fedha hawana taarifa nazo na ndio bahati mbaya sana iliyopo katika eneo hili lakini kama mtatumia wanasiasa, hao ni daraja lepesi sana la kuweza kuwafikia  watu hao,"Ameeleza Kikwete

"Ili jambo ukimwezesha diwani yeye atakuwa spika phone zetu, ukimwezesha mbunge  una hakika kabisa watu wataelewa hicho kitu kwani niwachache sana wanaofahamu kuhusu hizi asilimia 30 za manunuzi ya ndani na mtakapoondoka na maadhimio yenu moja ya eneo kubwa ambalo mnatakiwa muondoke nalo na kuufanya kuwampango kazi wa utekelezaji  wa majukumu yenu katika mwaka wa fedha 2025/2026 lazima  eneo la kutoa elimu liwe msingi namba moja kwenda kulifanyia kazi,"Amesisitiza

Amefafanua kuwa changamoto  hizo za uelewa mdogo na kwa baadhi ya wanufaika kuhusu utaratibu wa kushiriki katika zabuni ziwe msingi wa mipango ya utekelezaji katika siku zijazo na ni ahadi ya serikali kuendelea kuchukua hatua madhubuti kupitia mafunzo miongozo na ufuatiliaji wa karibu ili kuziondoa changamoto hizo.

Amesema kuwa wanapojipanga kutekeleza mipango ya kimaendeleo kibajeti katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 serikali itaendelea kuetekeleza na kuongeza usimamizi na ufuatiliaji kwa karibu katika utekelezaji wa asilimia 30 ya zabuni kwa makundi maalum ambapo ni wazi kuwa elimu zaidi inatakiwa.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 vijana walio katika umri wa miaka 15 hadi 35 wa Tanzania bara wanakadiriwa kufika milioni 21 sawa na asilimia 34.4 ya watanzania wote huku wenye ulemavu wakiwa ni  takribani watu milioni 5,251,729 sawa na asilimia 8.9 ua watanzania wote 

"Hii inatoa umuhimu wa kipekee kwa serikali kuwekeza kwa dhati kwa makundi haya kwa lengo la kukuza uchumi jumuishi ambapo kwa kutekeleza agizo la kisheria la kutenga asilimia 30 za zabuni za ununuzi wa umma kwa makampuni ya wazawa na makundi maalum, ambayo imeongeza ushiriki wa vijana na wenye ulemavu katika kuchakata zabuni ambapo katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 jumla ya vikundi 119 vilipata tuzo za zabuni zenye thamani ya shilingi bilioni 4.02 ikilinganishwa na vikundi 57 vya vijana vilivyopata  tuzo katika mwaka 2024/2025," Ameeleza

"Zabuni 143 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.2 kwa upande wa vijana zilitolewa ma kwa upande walemavu  vikundi vitatu vilipewa jumlabya zabuni 17 zenye thani ya shilingi  bilioni 1.01 hadi kufikia mwezi Mei 2025," Amefafanua.


Kwa upande wake mkurugenzi wa  mamlaka ya ununuzi  wa umma  Denis Simba amesema kuwa bajeti ya mwaka 2024/2025 ilikuwa takribani trilion 50 na 2025/2026 ni trilion 56.5 amapo kati ya asilimia 50 mpaka 70 ni ununuzi wa umma  ambapo kwa hesabu za kawaida eneo hilo la makundi maalum kabla ya kufika 2030 inweza likafikia takriban trilioni 5.

"Hii inamaana tutakuwa tumeongeza ajira, tumechochea ujasiriamali katika nchi kwasababu yale makundi yatajiunfa na kufanya biashara na serikali na vile vile tutakuwa tumeongeza wigo wa walipa kodi," Amesema Simba.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI