Header Ads Widget

FADHIL GAJILO ATIA NIA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo ameandika barua kwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa kusimama kwa muda nafasi yake ili kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama hicho.


Akizungumza  na waandishi wa Habari wakati akitangaza nia Ngajilo amesema kuwa amejipima na kuona ana uwezo na  sifa zote za kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini  na mipango ya kuwavusha wana Iringa anayo.

“Tupo katika mwaka wa Uchanguzi Mkuu mimi Fadhili  Fabian Ngajilo nimeona ni vema nikatangaza rasmi kuwa tarehe 28 ya mwezi huu  nitachukua  fomu ya kuomba kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia chama changu cha CCM na katika kueleza nia yangu hii tayari nilishaandika barua kwa chama changu kupitia  Katibu wa Mkoa kupisha kwa muda nafasi yangu ya  Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Iringa  kwasababu nimetia nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hili la  Iringa Mjini kupitia kwa  Chama Cha Mapinduzi , lakini pia nimefanya hivi kwasababu  nina tumia haki yangu ya kikatiba ya kugombea nafasi hii ya ubunge nikiwa nasifa zote za kiongozi wa Jimbo na mwakilishi wa wananchi Bungeni nimejipima kwa vigezo vyote nimeona vinatosha mpaka vinamwagika ’’

Pia Ngajilo ameongeza kuwa Mkoa huo wa Iringa unahitaji Sauti ya watu ambayo itasema jambo Bungeni au popote na likaweza kusikilizwa na kufanyiwa kazi ukizingatia vita ya kiuchumi inahitaji watetezi na watu wenye uwezo wa kujenga hoja za kuvutia miradi na uwekezaji katika sekta ya viwanda,biashara,na sekta ya utalii lakini pia sauti hii inahitajika kuwaunganisha wana Iringa kwa rika,jinsia na Imani zao yaani watoto,vijana,wazee, wanaume na wanawake.


Aidha Ngajilo ameelezea faida mbalimbali alizozipata pindi alipokuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi na  jinsi nafasi hizo zitakavyoweza kusaidia katika kuleta maendeleo kwa wana Iringa.


“Chama changu cha Mapinduzi kimenilea katika nafasi mbalimbali ikiwa kwasasa ni Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa (UVCCM) lakini pia niliwahi kuwa Mwenyekiti Jumuiya ya vijana Mkoa wa Iringa kutoka 2008 mpaka 2012 lakini pia nimehudhuria vikao mbalimbali vya Chama vya Mkoa pia Kitaifa nimehurudhia mikutano mbalimbali na kwa hilo nina uzoefu wa kutosha kuweza kutumia uzoefu huo kuleta mabadiliko katika Mkoa huu.

Hata hivyo Ngajilo ametumia nafasi hiyo kuweza kuelezea  fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa huo na namna mbavyo zikitumiwa vizuri zinaweza kuleta maendeleo kupitia uwepo wa kiongozi mwenye ubunifu,msikivu na mwenye uzalendo wa kweli katika kuleta mabadiliko.

“Mkoa wa huu unahitaji viwanda ili tuweza kuongeza mzunguko wa fedha moja ya changamoto kubwa ya uchumi katika mkoa wa Iringa ni mzunguko wa fedha lazima tuwekeze katika viwanda na mimi nishukuru ilani yetu  ya uchaguzi mpya ya chama imesema  wazi serikali itawekeza katika viwanda vikubwa na viwanda vidogo  na  tunamhitaji Ngajilo aweze kusukuma ajenda hizo ili tuweze kuwa na viwanda na uwezo huo ninao”


Kwa upande mwingine Ngajilo amegusia uwepo wa vivutio vya utalii katika Mkoa wa Iringa na kueleza kuwa agenda ya utalii katika mkoa huo  ni muhimu sana katika kuendeleza sekta ya utalii.

“Agenda ya utalii kwa Iringa ni muhimu sana ukizingatia mji huu umezungukwa na vivutio vya utalii vingi kama Ruaha National Park, Kalenga na Uwanja wa ndege mzuri bila kusahau hali ya hewa uwepo wa makapuni ya Utalii na ukarimu wa wana Iringa hivi ni vigezo tosha kuvutia watalii wa kitaifa na kimataifa kuja katika mkoa huu na katika hili ubunifu unahitajika kutumika ili kuona namna ya kugeuza vivutio hivi kuwa fursa za uwekezaji na ajira.

Aidha kwa kuzingatia uwepo waTaasisi ya  Ngajilo Foundation na Ngajilo Cup (Vunjabei Cup) ambayo kwa miaka 15 imekuwa ikiendeshwa na Ngajilo kwa lengo la kuendeleza michezo na burudani ameeleza kuwa ameandaa mikakati madubuti ya kuleta heshima ya Iringa katika medani ya michezo.

“Mkoa wetu pia unahitaji mtu anayetambua maana ya kuweka mifumo ya burudani na michezo na mimi nikiwa kama mdau wa michezo nipo tayari kuwaunganisha wadau wa michezo ukizingatia ninaushuhuda wa kuonesha uwezo wangu kwa miaka 15 kwa kuendesha kombe la Ngajilo Cup (Vunjabei Cup) kupitia Taasisi yangu ya Ngajilo Foundation,Iringa yetu inahitaji timu ya Ligi Kuu na mimi nimejipanga kwa kuja na mikakati madhubuti ya kurudisha heshima ya Iringa katika medani ya michezo.


Ikumbukwe kwamba hii itakuwa ni mara ya Tatu kwa Fadhili Fabian Ngajilo kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hii ya Ubunge katika jimbo la  Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM ambapo alishiriki kwa mwaka 2010, 2020 na sasa 2025.


Jimbo la Iringa mjini kwa sasa linaongozwa na mbunge Jesca Msambatavangu ambae anamalizia kipindi chake cha miaka mitano

SIMULIZI CHINI ⬇️⬇️⬇️⬇️⬇️

.Mchepuko wa mume wangu ananifokea kwenye simu bila aibu! 

Naitwa Asma, nimekuja kugunudua kadiri miaka inavyozidi kusonga ndivyo ambavyo jambo la wanaume kuzisaliti ndoa zao linazidi kuonekana jambo la kawaida, wanawake wanaotembea na wanaume za watu wamekuwa hadi wanafikia hatua ya kujisifu kwa kuwakamata wanaume za wazao.

Hawa wanajiita nyumba ndogo na kwa sasa kuna wimbo maarufu unaokwenda kwa jina la hilo ambao wamekuwa wakitamba nao, wanaume wenyewe wanasema nyumba kubwa hainogi bila kuwa na nyumba ndogo. 

Huu ni mchezo hatari sana kwani sasa dunia imechafuka na magonjwa ni mengi, pia wanaume wanashindwa na kufanya mambo ya maendeleo katika famili zao kisa nyumba ndogo. 

Mume wangu naye aliingia katika tabia hiyo, alikuwa na nyumba ndogo ambayo ilikuwa imemteka kweli kweli, kuna wakati mume alikuwa anachelewa kurudi nyumbani. 

Siku moja nilimpigia simu yake anapokea huyo mwanamke wake na kuanza kunifokea na maneno makali ambayo huuchoma moyo wangu.

Nilishikwa na hasira ambayo hajawahi kunipata, niliamua kuchukua vitu vyangu na kurejea kwa wazazi wangu, niliwaeleza kuwa mume wangu amekuwa akichepuka sana. 

Asubuhi iliyofuata mama yangu aliniita pembeni na kuniambia hilo lisivunje ndoa yangu, akaniambia kuna mtu anaitwa Kiwanga Doctors kutokea Migori, Kenya anaweza kunisaidia. 

Basi akachukua simu yake na kunipatia namba yake, nilipiga pale pale mama akiwa anasikiliza, Kiwanga Doctors alinisikiliza kwa makini akaniambia huo ndio utakuwa mwisho wa mume wangu kuchepuka.

Niliendelea kukaa kwa wazazi wangu, baada ya siku tatu mume wangu alikuja nyumbani kwa ajili ya kuniomba msamaha, tulikaa kikao na wazazi wangu na akakiri mbele yao kuwa hawezi tena kurudia jambo hilo lilokuwa linanitia aibu maisha mwangu.

Kesho yake yule mchepuko wake alinipigia simu naye akiomba msamaha kwa kutembea na mume wangu huku akilia na kusema bila msamaha wangu anajiona atakafa, sikujua ni jambo gani hasa limempata. Kutokana ni mwanamke mwenzangu, niliingiwa na roho ya huruma na kuamua kumsamehe.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba  +255 763 926 750  au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI