Header Ads Widget

ASASI ZA KIRAIA KUKUTANA ARUSHA

  



Na Pamela Mollel, Arusha 


Asasi za kiraia (Azaki) za kirai inatarajia kuwakutanisha wadau wake zaidi ya 500 huku mada mbalimbali zikijadiliwa Kwa lengo la kusaidia jamii.


Aidha mkutano huo unatarajiwa kuanzia Juni 2 hadi 6 jijini Arusha huku ikikutanisha wadau mbalimbali kujadili dira ya maendeleo ya Taifa 


Hayo yameleezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, amesema kuwa katika wiki hiyo ya Azaki Arusha kutakuwa na majadiliano mbalimbali ambayo yote yanalenga kusaidia jamii.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa Kamati za Azaki, Nesia Mahenge, amesema wiki hiyo inalenga kuangalia changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye jamii


Alisema kuwa hii ni mara ya saba kwa asasi hizo kukutana na kujadili mambo mbalimbali ambayo yanalenga jamii.


"Sisi tutathmini changamoto na mafanikio ya mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Tanzania bara na Zanzibar, pamoja na kuweka mikakati ya kuzitatua hivyo tunavyokutana huwa tunajadili kwa pamoja"aliongeza.


Mahenge amesema Azaki zitatumia fursa hiyo kupanga mikakati ya kutafuta rasilimali na ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya jamii huku wakitoa mfano wa mataifa mengine yanayojifunza kutoka kwa mafanikio ya Tanzania 


Kwa upande wake Meneja mwandamizi mahusiano kutoka benki ya Stanbic,Dickinson Senzi anasema wanatarajia kutoa elimu kuhusu maswala ya kifedha kwa kuwa benki hiyo ni namba 3 na imekuwa ikiwahudumia watanzania na kutoa masuluhisho


Mwisho. 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI