Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani imeungana na taasisi zingine za vipimo duniani kuadhimisha Siku ya Vipimo kwa kufanya ziara ya ghafla kukagua vituo viwili vya Mafuta (Petro station) na kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo katika wilaya za Kibaha na Bagamoyo mkoani humo.
WMA mkoa wa Pwani wametumia siku hiyo kutoa Elimu ya vipimo sahihi kwa wadau wa vipimo ikiwemo kituo Cha mafuta Msolwa Chalinze, kiwanda Cha kuzalisha vyakula vya mifugo Cha animal care kilichoko Kibaha mjini na kituo Cha mafuta Cha Petro Africa kilichoko Misugusugu wilayani Kibaha.
Afisa vipimo mwandamizi mkoa wa Pwani Abeid Jalala amesema maadhimisho ya siku ya Vipimo duniani huadhimishwa Mei 20 kila mwaka ambapo sasa ni mwaka wa 150 tangu kuanza maadhimisho hayo May 20 mwaka 1875 wametoa wito kwa wadau wa vipimo kuendelea kutumia vipimo vilivyohakikiwa kwa Faida yao na ya mlaji wa mwisho.
Meneja kituo Cha mafuta Msolwa Chalinze Juma Munis amesema Wakala wa Vipimo WMA wamekuwa wakiwatelmbelea mara kwa mara kutoa elimu na kuhakiki mizani yao kwani wana jukumu la kuhakikisha kwamba vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine ni sahihi, kulingana na Sheria ya Vipimo.
Baadhi ya wadau wa vipimo wameishukuru WMA kwa kuendelea kutoa Elimu ya vipimo..
++++++
0 Comments