Header Ads Widget

WIZARA YA AFYA YAONYA CORONA BADO IPO.

 


DAR ES SALAAM: WIZARA ya Afya imesema kuwa ugonjwa wa UVIKO-19 bado upo nchini, sambamba na magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo leo, Mei 20, 2025, imesema kumekuwa na ongezeko la visa vya UVIKO-19 kutoka asilimia 1.4 mwezi Februari hadi asilimia 16.3 mwezi Machi, na kufikia asilimia 16.8 Aprili mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa kwa lengo la kuutahadharisha umma kuhusu hatari ya magonjwa yanayoenea kwa njia ya hewa pamoja na yale yanayoenezwa na mbu, huku ikisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kujikinga.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kuanzia Januari hadi Aprili 2025, kumekuwa na ongezeko la tetesi kuhusu magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa, hasa katika Jiji la Dar es Salaam. Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Afya imeendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu na kutoa taarifa za kila siku kuhusu magonjwa ya milipuko.

"Ugonjwa wa UVIKO-19, ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini mwezi Machi 2020, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa. Hata hivyo, kuanzia Februari hadi Aprili 2025, kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya maambukizi kutoka asilimia 1.4 hadi asilimia 16.8," imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Afya imetoa wito kwa wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya njia ya hewa.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI