Na Matukio Daima App
DAR ES SALAAM.Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo-Bara, Isihaka Mchinjita amemtangaza Wakili Peter Madeleka kuwa mwanachama mpya aliyejiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Madeleka tayari amekabidhiwa kadi ya uanachama wa chama hicho pamoja na katiba ikiwa ni ishara ya kuwa mwanachama wa chama hicho.
Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 20, 2025 makao makuu ya chama hicho, Magomeni, ambapo Isihaka amemtaja Wakili Madeleka kama mpigania haki kwa wananchi wote.
Wakili Madeleka amesema lengo la kujiunga na ACT Wazalendo ni kuimarisha nguvu katika upinzani na kutoa matumaini kwa Watanzania kufika wanakotaka.
"Hitaji la kuwa na demokrasia, utawala unaoheshimu haki za binadamu ni vita kama vita vingine na vita hivi lazima vipiganwe kwa njia nyingi," amesema.
MWISHO.
0 Comments