Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mha. Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Andreas Bjelland Eriksen - Waziri wa Hali ya Hewa na Mazingira wa Norway.
Mazungumzo hayo yalilenga ushiriki wa Tanzania katika COP30 na majadiliano kuhusu taka za Plastiki, yalifanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Oslo, nchini Norway.
Akizungumza kuhusu jitihada za Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, Waziri Masauni alimweleza Bw. Eriksen kuwa Tanzania imejipanga kuhifadhi Mazingira kwa kuja na mipango na makatazo mbalimbali ikiwepo agenda ya Nishati Safi ya kupikia.
Tanzania imepanga kupunguza matumizi ya Nishati isiyo salama ya kupikia na kuhakikisha kuwa kufikia 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wakitumia nishati Safi ya Kupikia.
Aidha Waziri Masauji, alimweleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye kinara wa Nishati Safi ya Kupikia Afrika na Duniani kote.
Waziri Masauni aliendelea kuelezea kuwa Tanzania imekuwa na program za mpito kwa kutoa makatazo ya matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kuanzia 2024.
Aidha Tanzania imetoa katazo la matumizi ya plastiki (Vibebeo) na kuainisha tofauti ya vibebeo na vifungashio.
Akizungumza Waziri Eriksen amesema kuwa COP30 ni fursa adhimu kwani kila nchi duniani itapata fursa ya kuwasilisha taarifa yake ya tatu ya ‘Nationa Determined Contribution’-NDC.
“Nina imani kuwa pamoja na taarifa hizo kuna baadhi ya nchi zitakuwa zimetimiza adhma zao na baadhi kutotimiza hivyo COP30 itatoa fursa ya kuona nini kifanyike ili kuziba mapengo hayo”, amesema Bw. Eriksen.
Aidha ameleza kuwa kwa kufanya kazi kwa mashirikiano baina ya mataifa mbalimbali ni matarajio yake kuwa ahadi ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi- ‘Adaptation Finance’ itaongezeka mara tatu - ‘Triplering Adaptation fund’.
Serikali ya Norway inafanyia kazi upatikanaji wa fedha kwa ajili ya masuala ya Mazingira na tayari wana Mfumo wa utekelezaji wa Artice 6 ambao unawasaidia katika utekelezaji wa miradi jumuishi, ili kuwa na lengo la pamoja na hivyo kuibua fursa mpya.
Article 6 inalenga kuibua fursa mpya. Hivyo Tanzania ikiwa mwenyekiti wa ‘ African Group of Negotiators’- AGN inaweza tumia fursa hiyo kuzishawishi nchi hizo kutambua fursa zilizopo na kuzitumia kwa mapana zaidi.
Akizungumzia taka za plastic Waziri Eriksen ameeleza kuwa kuna umuhimu wa majadiliano ya kina kuhusu taka za plastiki kwani zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku. Hivyo ni muhimu mataifa yakashirikiana kukabiliana na janga hili.
0 Comments