Header Ads Widget

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA DRC AHUKUMIWA MIAKA 10 KWA TUHUMA ZA RUSHWA

 

Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amehukumiwa kifungo cha miaka kumi cha kazi ya kulazimishwa kwa kosa la rushwa.

Augustin Matata Ponyo alipatikana na hatia ya ubadhirifu wa takribani $245m (£182m) za fedha za umma na Mahakama ya Kikatiba ya Congo siku ya Jumanne, pamoja na Deogratias Mutombo, gavana wa zamani wa benki kuu ya DR Congo.

Wakili wa Matata aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba uamuzi huo haukuwa wa haki na ulichochewa kisiasa.

Sehemu ya fedha zilichukuliwa kutoka kwenye maendeleo makubwa ya kilimo yaliyokusudiwa kukabiliana na uhaba wa chakula nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI