Header Ads Widget

WALIOBADILI JINSIA WAZUIWA KUSHIRIKI KATIKA KRIKETI ZA WANAWAKE UINGEREZA

 


Bodi ya Kriketi ya Uingereza na Wales imebadilisha kanuni zao kwa watu wanaobadili jinsia

Wanaume waliobadili jinsia na kuwa wanawake wamezuiwa kushiriki katika michezo yote ya kriketi ya wanawake, imetangaza Bodi ya Kriketi ya Uingereza na Wales (ECB).

ECB inasema "ni wale tu ambao jinsia yao ya kibaolojia ni wanawake" ndio wataweza kushiriki katika kriketi ya wanawake na wasichana.

ECB inasema wanaume na wavulana waliobadili jinsia kuwa wanawake wanaweza kuendelea kucheza katika mechi za kriketi za mchanganyiko.

Mabadiliko ya sera yanafuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza tarehe 15 Aprili ambayo ilitoa ufafanuzi wa kisheria kwamba mwanamke ni ile jinsia ya kibaolojia.

Uamuzi huo unafuatia tangazo la Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) siku ya Alhamisi kwamba waliobadili jinsia hawataweza tena kushiriki katika soka la wanawake nchini Uingereza kuanzia tarehe 1 Juni.

Kanuni ya awali ya ECB ni kwamba waliobadili jinsia ambao walivuka balehe kama wanaume hawastahiki kushiriki katika ligi ya kriketi ya daraja la juu ya wanawake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI