Header Ads Widget

WAKILI SOSTEN MBEDULE: TUNAMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KWA KUTEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM

 

                kada wa CCM wilaya ya Iringa vijijini wakili Soste Mbedule 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoa wa Iringa, Wakili Sosten Mbedule, amempongeza kwa dhati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ndugu Salim Abri Asas, kwa heshima ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

"Kuwa uteuzi huo ni sahihi na umekuja wakati sahihi zaidi "

Katika salamu zake za pongezi, Wakili Mbedule amesema uteuzi huo ni wa kihistoria na wa kipekee, kwani siyo tu kwamba ni heshima kwa Asas binafsi, bali pia ni fahari kubwa kwa wanachama wote wa CCM mkoa wa Iringa ambao wamejengewa heshima na kuaminiwa kupitia uteuzi huo uliofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Matukio Daima Media, Wakili Mbedule alisema kuwa uteuzi wa Asas kuwa mjumbe wa Kamati Kuu unaashiria imani kubwa aliyonayo Rais Dkt. Samia kwa kada huyo, na kwamba wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa wameupokea kwa furaha na matumaini makubwa ya maendeleo zaidi ya chama chao.

“Uteuzi huu haujaja kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya uaminifu, uchapakazi na moyo wa kujitolea kwa Salim Abri Asas katika kulitumikia na kulijenga chama chetu. Tumekuwa tukimuona akiwa mstari wa mbele kusaidia shughuli za chama na jamii kwa ujumla hii ni heshima kwetu sote wana CCM wa Iringa,” alisema Wakili Mbedule.


Ameongeza kuwa Asas ni mtu anayejitoa kwa vitendo na mara zote amekuwa akifikiria namna ya kuhakikisha CCM inazidi kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi mbalimbali. 


Alisema kuwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha chama ngazi ya wilaya na mkoa ni jambo ambalo halina shaka na linastahili kutambuliwa kitaifa.

Wakili Mbedule pia alisisitiza kuwa uteuzi wa Asas uwe chachu kwa wana CCM wote mkoani Iringa kuendelea kushikamana, kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama, na kuhakikisha wanampigia kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kishindo pamoja na wagombea wote wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

“Ni wajibu wetu sasa kumuunga mkono ndugu Asas na kuhakikisha tunamfanya aheshimike zaidi kupitia ushindi mkubwa wa chama chetu kura nyingi kwa Rais Samia na CCM kwa ujumla ni njia bora ya kuonyesha kuwa mkoa wa Iringa unathamini uongozi wake na unautambua mchango wake kwa chama,” alihitimisha Wakili Mbedule.

Kwa ujumla, Wakili Mbedule alisisitiza kuwa uteuzi wa Salim Abri Asas ni motisha kwa makada wengine wa chama kujituma zaidi, kujenga umoja, na kufanya kazi kwa uaminifu kwa ajili ya CCM na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI