Virusi vya West Nile vimegunduliwa kwa mbu wa Uingereza kwa mara ya kwanza, maafisa wa afya wa Uingereza wanasema.
Hatari kwa umma kwa ujumla ni "chini sana" na ingawa virusi hivyo vinaweza kuwafanya watu kuwa wagonjwa sana katika hali ambayo ni nadra, hakuna ushahidi kwamba virusi hivyo vinaenea kwa mbu nchini Uingereza, Shirika la Usalama la Afya la Uingereza (UKHSA) liliongeza.
Virusi hivyo vinavyoenezwa kupitia mbu wanaouma ndege, vinapatikana katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na bara la Ulaya.
Hadi kufikia sasa, hakujawa na visa vya binadamu vya virusi vya West Nile vilivyopatikana nchini Uingereza - ingawa kumekuwa na visa saba vya ugonjwa huo vinavyohusishwa kusafiri kwenda nchi zingine tangu 2000.
Virusi vya West Nile vimeenea katika maeneo kadhaa duniani, ikiwa ni pamoja na sehemu za Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Ulaya, na vimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.
0 Comments