Na Matukio Daima Media
Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kupongezwa kwa kasi na ubora wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi wa kada zote nchini.
Wito umetolewa kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kutangaza mafanikio hayo makubwa ambayo yanaendelea kuonekana katika kila pembe ya nchi.
Akizungumza na Matukio Daima Media, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, Jasmin Ng’umbi, amesema vijana wanayo nafasi kubwa na ya kipekee ya kuendelea kuwa mabalozi wa maendeleo yanayoletwa na serikali ya CCM.
Jasmine alisema kuwa licha ya kazi nzuri ya serikali kujionyesha yenyewe kwa matokeo chanya kwa wananchi, bado ipo haja kwa vijana kutumia sauti zao na majukwaa waliyonayo katika kuyatangaza mafanikio hayo ili kuiongezea nguvu serikali ya awamu ya sita.
“Tunaona kazi nzuri inayofanyika, miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa nchi nzima ni ushahidi tosha.
Kuwa kila Mtanzania anashuhudia na kunufaika na jitihada hizi ni jukumu letu vijana, hususan sisi wa UVCCM, kuendelea kuwaeleza wananchi kazi hizi, kwani wapo wapinzani wachache ambao kazi yao kubwa ni kupotosha ,Nguvu yao ya upotoshaji inapaswa kushindwa kwa nguvu ya ukweli,” alisema Jasmin Ng’umbi.
Akaongeza kuwa kazi ya kutangaza mafanikio ya serikali si ya kuachiwa viongozi wa juu pekee, bali inapaswa kuwa ajenda ya kila kijana mzalendo anayeona manufaa ya maendeleo yanayokuja kupitia miradi hiyo.
Alisema kuwa miradi inayotekelezwa siyo tu ya kitaifa kama reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa barabara kuu, na miradi ya umeme, bali pia miradi ya kijamii inayofanyika kwenye vijiji, kata na tarafa imeendelea kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi.
Ng’umbi alisisitiza kuwa miradi hiyo imefungua fursa nyingi za ajira na biashara, huku vijana wakinufaika kwa kutoa huduma mbalimbali kama usafirishaji, biashara ndogo ndogo, na huduma za kijamii.
“Miradi hii imekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya watu wetu ajira zimeongezeka, vipato vimeimarika, hali ya maisha imeanza kubadilika huu ni ushahidi kuwa serikali yetu inajali watu wake,” alibainisha.
Katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao, Ng’umbi alisema ni muhimu kwa vijana wa CCM na UVCCM kwa ujumla kuhakikisha hawachoki kusema ukweli kuhusu mafanikio haya na kuwaelimisha wananchi dhidi ya upotoshaji unaoenezwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo.
“Tuwe mstari wa mbele kila mara. Tuendelee kuwaambia watu kuwa haya yote tunayoyaona si ya bahati mbaya, bali ni matokeo ya utekelezaji makini wa Ilani ya CCM. Tusikubali kurudi nyuma, tusikubali propaganda kuwachanganya wananchi,” alisisitiza.
Kwa ujumla, Jasmin Ng’umbi aliwataka vijana kote nchini, hasa ndani ya UVCCM, kuchukua nafasi yao kama nguzo ya chama na taifa, kwa kuhakikisha wanatumia sauti zao, taaluma zao, na vipaji vyao kutangaza kazi nzuri za maendeleo.
Alisema huu si wakati wa kunyamaza, bali ni wakati wa kusema, kushuhudia na kusambaza mafanikio haya kwa kila mtanzania.
Jasmine aliomba vijana kuendelea kuwa sehemu ya mabadiliko na mafanikio, kwa kuisemia serikali ya CCM Kwani kwa kufanya hivyo kunasaidia kuimarisha mshikamano na imani ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi na serikali yake.
1 Comments
Wewe ndiye kitu bora zaidi ambacho kimewahi kunitokea, ulimrudisha mume wangu wakati nilidhani hakuna kitakachotokea kwa sisi kuwa pamoja tena. Utakuwa na baraka na maombi yangu kila wakati kwa spell hii yenye nguvu ambayo umenifanyia na mume wangu kuwasiliana nayo.
ReplyDeleteHii hapa Dr Dawn Whatsapp number: ( +2349046229159 ) kwa wale ambao wana matatizo katika mahusiano/ndoa/ maisha,
Hata ikiwa ni maswala ya uzazi, kesi ya Curt, nambari za kushinda bahati nasibu, E.T.C.
DR Dawn Whatsapp: +2349046229159
Barua pepe dawnacuna314@gmail.com