Header Ads Widget

UTANDAWAZI, MILA ZA KIGENI VINACHANGIA UKATILI NCHINI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

VIONGOZI wa dini na viongozi wa mila mkoani Kigoma wamesema kuwa jamii kuacha kuishi kwa kufuata misingi ya dini, mila na desturi za Mtanzania kumechangia kuendelea kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto mkoani Kigoma.

Viongozi hao wamesema hayo  katika Kikao kazi na viongozi wa dini, viongozi wa kimila, watu maarufu na wawakilishi wa vijana juu ya namna ya kuleta mabadiliko katika mila na desturi na kuondoa mila kandamizi kwa lengo la kupunguza ukatili wa kijinsia  kilichoitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UN WOMEN) kwa ufadhili wa Serikali ya Norway.

Akizungumzia changamoto hiyo Mchungaji wa kanisa EAGT wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma,Leonald  Kibuguzo alisema kuwa nyumba za ibada zipo na waumini wanajaa makanisani na misikitini lakini wengi wao hawaishi mafundisho yanayotolewa kwenye nyumba za ibada za kutaka watu kuishi kwa Amani na upendo ambayo ndiyo msingi wa kutokomeza ukatili.

Akifungua mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya mji wa Kasulu, Azizi Nurfusi alisema kuwa viongozi wa dini na wazee wa mila na wazee maarufu kwenye jamii bado wanayo nafasi kubwa ya kuiasa jamii na jamii kuondokana na vitendo vya ukatili.

Nurufus alisema kuwa kwa kutumia nafasi yao viongozi hao wanaweza  kuweka mkakati ambao utasaidia kuishauri serikali kutafuta namna bora ya jamii kuishi na kuondokana na changamoto za vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee mkoa Kigoma, Mbonipa Bisama alisema kuwa utandawazi na maendeleo ya teknolojia yamekuwa yakitumika vibaya kutokana na watu wengi kuacha mila na desturi za Watanzania na kufuata mila,desturi na tamaduni za nje.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI