Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ameeleza kuwa kuwa msisimko wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu serikali sasa ni muda na inapaswa kukaa chini na kuzungumza ili kuepusha migongano iliyopo kwa kushauriana namna gani yanaweza kutatulika.
Akizungumza katika kongamano la kitaifa kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025 Mei 3,2025 lililofanyika jijini Dar es Salaam, Warioba ameeleza kuwa moja ya changamoto ni kanuni mpya zinazotaka vyama vya siasa visivyosaini kanuni hizo kuzuiwa kushiriki uchaguzi, bila kuweka wazi muda wa utekelezaji wake.
Warioba pia amesisitiza umuhimu wa kusawazisha haki na amani wakati wa uchaguzi, akionya kuwa kupuuzia upande mmoja kutasababisha migogoro
Aidha ameongeza kuwa Ibara ya 8 ya Katiba inayosema chimbuko la madaraka ni wananchi, na kushiriki kwao ni haki ya kikatiba. pia ametaja changamoto zilizojitokeza kwenye chaguzi zilizopita kutokana na kanuni za mwaka 2019 ambazo ziliondoa wagombea kwa masharti yasiyokuwamo kwenye katiba, jambo lililorudiwa tena mwaka 2020 na 2024 na kusisitiza zisijirudie.
"Wapo watu wengi wanazungumzia amani lakini hakuna msisitizo kwenye haki, na wengine wanatoa haki bila kuipa kipaumbele amani visipozingatiwa kutakuwa na matatizo." Jaji warioba
0 Comments