Header Ads Widget

MISINGI YA UCHAGUZI NI IBARA YA NANE YA KATIBA

 

"Zoezi la uchaguzi ndio zoezi linaloanza moja kwa moja kwenye Ibara ya 8 ya Katiba, pale tunaposikia mamlaka inatoka kwa watu hapo unazungumzia mwanzo wake ni huku kwenye uchaguzi, kwahiyo ili kulinda Ibara hiyo ya 8 tunahitaji uhuru wa mchakato, uhuru wa uwazi, tunahitaji uchaguzi wa uwazi kwa maana ya uwajibikaji, changamoto tunazozikuta ni muhimu zitatuliwe mezani" -Wakili Mwabukusi

"Kwahiyo tunachozungumza hapa ni kwamba tunahitaji hatua madhubuti, za uhakika na tunahitaji time flame, tunahitaji kuwa na matatajio yanayokubalika, inapofikia hatua ya sehemu kubwa kukosa imani na mifumo ya uchaguzi hatutakiwi kusubiri, kuna mambo tusipochukua hatua madhubuti na kwa wakati tunaweza kuligawa Taifa" -Wakili Mwabukusi

"TLS sio ndege mpitaji, tupo tunaona, sisi ni taasisi ya kitaaluma, tumeleta mada mbalimbali, hapa tunazungumza kwa uwazi, bila hofu kwani ni haki yetu ya kisheria na Kikatiba ili mwisho wa siku tutoke na yale tunayoona ni ya msingi na yanayostahili basi tushauriane ili zoezi letu la uchaguzi liwe ni lenye uadilifu, uwazi, uwajibikaji na lenye kuleta matokeo yaliyotarajiwa kupitia sanduku la kura na sio njia nyingine za mkato" -Wakili Mwabukusi

Ni sehemu ya yale aliyozungumza Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi kwenye kongamano la Kitaifa kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania, kongamano liloloandaliwa na TLS ambalo limefanyika leo, Jumamosi Mei 03.2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI