Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, (CHADEMA) Tundu Lissu ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uchochezi, amegoma kula akiwa gerezani kama ishara ya kutaka haki itendeke.
Wakili wa Tundu Lissu, Peter Kibatala amebainisha kuwa atasusia kula hadi pale atakapoona haki inatendeka ‘’Anaanza kususia kula chakula, sio kwasababu nyingine, anataka haki itendeke’’ alibainisha Kibatala wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mbali na Shitaka la uhaini anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu kuharibiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kutumika kwa Polisi kuipa kura na Majaji kutotenda haki kwa kuwa ni wateule wa Rais.
Lissu alikamatwa mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma, kusini mwa Tanzania mwezi uliopita.
Akiendelea kunadi msimamo wa chama hicho wa 'No Reforms, No Election, No Reforms, No Election, ni msimamo wa kisera wa chama hicho uliopitishwa na Kamati Kuu katika kikao chake cha Disemba 2-3, 2024 unaodai kuwa CHADEMA haitoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kama hakutafanyika mabadiliko ya kimfumo katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba, sheria, na kuhakikisha kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.
Zaidi Lissu na chama hicho unaeleza kwamba uchaguzi hautafanyika nchini humo kama marekebisho wanayodai hayatafanyika. Kesi dhidi yake inatarajiwa kusikilizwa tena may 6.
0 Comments