Header Ads Widget

TFS SAO HILL WAFANYA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA TARAFA YA NNE SHAMBA LA MGOLOLO

Mnamo Mei 14, 2025 Wahifadhi kutoka TFS-Shamba la Miti sao Hill wametembelea na kukagua ukarabati wa miondombinu ya barabara unaoendelea katika Tarafa ya Nne ya Shamba Mgololo, Safu ya Simbi.

Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa mawasiliano ya barabara zilizopo ndani ya msitu yanaendelea  kuwepo ili kuhakikisha  shughuli za shamba na zile za watumiaji wa barabara hizo ambao ni wavunaji wa miti wanaosafirisha malighafi za miti wanapita katika barabara hizo bila vikwazo vyovyote.

TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza ili kuhakikisha wadau wanaovuna malighafi katika Shamba wanafanya shughuli hiyo kwa wakati na hivyo kupekelekea uvunaji na usafirisha wa malighafi unafanyika bila vikwazo, na kupelekea wadau hao kufanya shughuli zao kwa wakati za kujipatia kipato kwa kuvuna malighafi ya miti na pia serikali kukusanya mapato yake kwa wakati uliopangwa.

Shughuli mbalimbali zinaendele hapa TFS - Shamba la miti Sao Hii katika Tarafa zote nne (4) za shamba ikiwa ni pamoja na maandalizi ya bustani ya miche ya miti kwaajili ya msimu ujao wa upandaji na uvunaji wa malighafi ya miti katika kipindi hiki ambacho mvua katika baadhi ya maeneo zinaendelea kunyesha.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI