Header Ads Widget

SEA SENSE YATOA SIMU 33 ZA MFUMO MAALUM KWA BMU 11 MKURANGA WAKUSANYE DATA KIDIGITALI

 

Taasisi ya Sea Sense Tanzania imekabidhi simu janja 33 zenye mfumo maalumu wa kukusanyia wa takwimu na taarifa kidigitali za thamani ya zaidi ya shilingi milioni nane kwa lengo la kurahisisha usimamizi na utunzaji wa rasrimali za bahari katika vijiji 11 vya fukwe za pwani ya wilaya Mkuranga mkoani Pwani zenye ya zaidi ya shilingi milioni nane.

Akitoa taarifa ya utekelezwaji wa mradi Afisa Mradi wa Sea Sense Rone Mwapindi  huko wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati wa mafunzo ya kujengewa uwezo wa matumizi bora ya ukusanyaji wa takwimu na taarifa za kidigitali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Sea Sense kwa ufadhiri wa Blue Venture ya nchini Uingereza.


Amesema kwa miaka mitatu Sasa wamekuwa na mradi huo unaofadhiriwa na Blue Venture katika vijiji 11 wilayani Mkuranga mkoani Pwani lakini hasa ni.kutoka mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara.

Alisema hapo awali Wilaya ya Mkuranga haikuwa na vikundi vya usimamizi wa rasrimali za bahari na fukwe BMU katika Kila Kijiji hivyo imesaidia kuhakikisha rasrimali za bahari zinatunzwa na vikundi hivi Sasa vinajitegemea na kuhakikisha video nafanya shughili zake kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya uvuvi na kutoa mchango katika serikali za vijiji ikiwa ni pamoja na ulinzi shirikishi na shughili za kijamii pia.


Swaliha Msomi Katibu wa kikundi cha usimamizi na utunzaji wa rasrimali za bahari BMU Kisiju Pwani alisema pamoja na mafunzo waliyopata lakini pia wanahitaji vifaa zaidi na mafunzo kwani wengi wao hawawezi kuzamia baharini kufanya dolia zenye ufanisi wa kukusanya takwimu na taarifa za chini ya maji na kupanda matumbawe baharini.

Alisema baada ya mafunzo hayo watatoa takwimu sahihi na kwa wakati tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo zilikuwa duni hasa kliliwawia ngumu zaidi kipindi cha mvua kwani taarifa nyingi zilikuwa zinaharibika.


Mshiriki wa BMU ya Koma Kisiwani Azani Abdallah aliishukuru taasisi ya Sea Sense kwa mafunzo mbalimbali na uwezeshaji wanaotoa kwa BMU nchini kwani jamii imeaanza kuelewa ambapo jamii imeaanza kubadilka usalama upo na mazingira yapo salama na uharibifu unaanza kunapotea.

Alisema bado jukumu la kuelimisha watu linahitajika ili waelimike na wakubali kuzingatia utunzaji wa mazingira ya ukanda wa Pwani ya bahari.

Katibu wa Wasimamizi wa raslimali za bahari BMU Mdimuni wilayani Mkuranga Juma Ngunde amesema ulkusanyaji wa takwimu na taarifa kidigitali unatunza muda na unarahisisha uhakiki wa taarifa tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo taarifa zilikuwa zinaweza kuharibika kwasababu mbalimbali.


"Kwa mfano kipindi cha mvua taarifa zilikuwa zinaweza kuharibika kwasababu ya kuingia maji pia kwa upande digitali ni rahisi hata kufanya marekebisho ukikosea kuweka jambo". 

Alisema taasisi ya Sea Sense imewasaidia namna ya utunzaji wa mazingira, utunzaji wa mazalia ya samaki kuwa bora kwani wao walikuwa wanaona uvuvi ni jambo la kurithi tu bila kujali matunzo hivyo walivua bila ya kuwa na mpango wa utunzaji wa mazingira ya samaki na kusababishia mazao ya samaki kupungua nchini.

"Sea Sense wametufundisha kuhusu namna ya kuwa na uvuvi endelevu na mwenendo wa bahari elimu inayotusaidia kuwa na ongezeko la mazalia ya samaki tofauti na tulivyokuwa tukivuna kiholela" alisema Ngunde.

"Hatukujua kwamba kuna baadhi ya mambo ukiyafanya baharini baadhi ya samaki wanapotea baharini kwahiyo Ile elimu imetupa faida sana sisi wavuvi"

Akifunga mafunzo hayo Katibu tawala wa Wilaya ya Mkuranga Omary Mwanga ameshukuru kwa mafunzo na simu hizo kwaajili ya vikundi vya usimamizi wa rasrimali za bahari BMU hizo ambapo aliwataka Wana vikundi hao kuzitunza na kuzituma kwa matumizi yaliyokusudiwa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI