Header Ads Widget

RC MTAMBI AIPONGEZA AZANIA BENK IKITOA MCHANGO WA MEZA NA VITI 300 KWA SHULE ZA SEKONDARI MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi  ameipongeza Benki ya Azania kwa kutoa meza na viti 300 kwa shule za sekondari katika jimbo la Musoma mjini.

Meza na viti hivyo vimetolewa na benki hiyo leo aprili 30 2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo katika kuunga mkono juhudi za serikali na kutimiza ombi la mbunge wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema mchango wa benki hiyo kwenye sekta ya elimu ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuungwa mkono na wadau wengine.


Licha ya kuipongeza na kuishukuru benki hiyo ameishukuru pia taasisi ya Nyansaho Foundation ambao pia wameahidi kuchangia upatikanaji wa madawati, meza na viti kwaajili ya shule za jimbo la Musoma mjini.

Amesema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo na sio kwa jimbo la Musoma mjini pekee bali mkoa mzima wa Mara.

" Hapa nimepokea madawati,viti na meza jumla ya 600 kutoka kwa mbunge Mathayo,Azania benki napenda kuwapongeza sana na kuwashukuru.


" Kupitia hafla hii nitoe wito wa kuhakikisha mkoa wa Mara hakuna mtoto anayekaa chini na suala la chakula shuleni liwe suala la lazima kwa wanafunzi",amesema.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi  meza na viti hivyo meneja wa benki hiyo tawi la Serengeti Elizabeth Koboko amesema wametimiza ombi la mbunge wa jimbo la Musoma mjini la kuchangia meza na viti hivyo.

Amesema Azania benki inatambua umuhimu wa elimu na namna serikali inavyofanya jitihada hivyo kutimiza ombi la mbunge huyo ili wanafunzi wake na kusomea sehemu sahihi..

Meneja mahusiano wa benki hiyo tawi la Serengeti Baraka Nyamhanga ɓamesema wametumia milioni 14 kutengeneza viti na meza hizo na kuahidi kuendelea kushiriki matukio ya kijamii kila wanapopata nafasi.

Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema hiyo ni awamu ya kwanza ya kukabidhi ikiwa ni mchango wake na wadau na shughuli hiyo itaendelea.

Amesema lengo ni kuhakikisha jimbo la Musoma mjini hakuna mtoto anayekaa chini na kuwashukuru wadau wanaochangia ikiwemo benki hiyo ya Azania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI