Header Ads Widget

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN: KIONGOZI MWAJIBIKAJI, MMPENDA HAKI NA DEMOKRASIA


Tangu kuingia madarakani mwaka 2021, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha uongozi wa kipekee unaojali haki, maridhiano na ustawi wa demokrasia nchini Tanzania. Hatua alizochukua zimeleta matumaini mapya kwa Watanzania na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa.

Alipochukua madaraka, mikutano ya vyama vya siasa ilikuwa imepigwa marufuku kwa zaidi ya miaka sita. Leo hii, vyama vyote vina uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara na kuzunguka nchi nzima kwa kadri ya uwezo wa kila chama– hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa waliokuwa wamekimbilia uhamishoni kwa hofu ya usalama wao walirudi nyumbani kwa amani, na sasa wanaendelea kushiriki katika shughuli za kisiasa bila bughudha.

Katika sekta ya habari, Rais Samia alikuta hali ya hofu na mashaka pamoja na viongozi woga. Hata hivyo, kwa maamuzi yake ya kijasiri, vyombo vya habari sasa vinafanya kazi kwa uhuru na uwazi mkubwa. Vituo vilivyokuwa vimefungwa vimeruhusiwa kurejea hewani.

Aidha, Rais Samia alichukua hatua madhubuti kuhusu kesi za muda mrefu, hasa zile zilizoonekana hazina ushahidi unaojitosheleza. Kesi nyingi zilifutwa ikiwemo za viongozi wa upinzani.

Si hayo tu – alifungua akaunti za benki za wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa bila maelezo ya kutosha, na hivyo kurudisha hali ya biashara na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Kwa haya yote na mengine mengi, Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa ni kiongozi anayejali haki, anayeheshimu demokrasia na aliye tayari kusikiliza na kushirikiana na kila Mtanzania. Ni mfano wa kiongozi wa kisasa anayechagiza maendeleo kwa maridhiano na maelewano.

Makala hii imeandikwa Na. Japhari Saidi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI