Header Ads Widget

NETANYAHU: TUTASITISHA KAMA HAMAS ITAWAACHILIA MATEKA NA KUWEKA SILAHA CHINI

Waziri Mkuu wa Israel amejibu kauli ya pamoja kutoka Uingereza, Ufaransa na Canada.

"Kwa kuitaka Israel ikomeshe vita vya kujihami kwa ajili ya maisha yetu kabla ya magaidi wa Hamas kwenye mpaka wetu kuangamizwa, na kwa kutaka taifa la Palestina, viongozi wa London, Ottawa na Paris wanatoa zawadi kubwa kwa shambulio la mauaji ya halaiki dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7 huku wakikaribisha ukatili zaidi wa aina hiyo," anasema.

Anaongeza: "Vita vinaweza kumalizika kesho ikiwa mateka waliosalia wataachiliwa, Hamas itaweka chini silaha zake, viongozi wake wauaji watahamishwa na Gaza kuondolewa kijeshi.

"Hakuna taifa linaloweza kutarajiwa kukubali chochote kidogo na Israeli hakika hawatakubali. "Hivi ni vita vya ustaarabu dhidi ya unyama. Israel itaendelea kujilinda kwa njia za haki hadi ushindi kamili upatikane."


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI