Header Ads Widget

NETANYAHU ASEMA ISRAEL ITADHIBITI ENEO LOTE LA GAZA



Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema katika video mpya iliyowekwa kwenye akaunti yake ya Telegram kwamba Israel itachukua udhibiti wa Gaza yote na kuzuia Hamas kupora misaada inayoingia katika eneo hilo.

"Tunahusika katika mapigano - makali na makubwa - na kuna maendeleo. Tutachukua udhibiti wa maeneo yote ya Ukanda, ndivyo tutafanya," anasema kwenye video.

Akihutubia ukosoaji wa vizuizi hivyo, Netanyahu anasema imekuwa muhimu tangu kuanza kwa vita huko Gaza kwa Israeli kuzuia njaa "kwa mtazamo wa vitendo na wa kidiplomasia". "Kwa ufupi, wengine hawatatuunga mkono; hatutaweza kukamilisha kazi ya ushindi," anasema.

"Kwa hivyo, tuliamua kutoa msaada mdogo wa kibinadamu wakati wa vita. Hatua hiyo inajiri baada ya serikali ya Israel kusema itaruhusu kiasi "cha msingi" cha chakula kuingia Gaza kufuatia mzingiro wa wiki 11.

Je, kizuizi cha Israeli ni nini?

Kama tumekuwa tukiripoti, Israel imetangaza kuwa itaruhusu "kiasi cha chakula" kuingia Gaza baada ya kuziba eneo hilo kwa wiki 11.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, Israel imezuia shehena zote za misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya matibabu, kuingia Gaza.

Uzuiaji huo umelaaniwa na viongozi mbalimbali na mashirika ya misaada, huku Israel ikikabiliwa na shinikizo la kutaka kuondoa.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya "hatari kubwa" ya njaa kwa Wapalestina milioni 2.1 wanaoishi Gaza.

Mashirika mengine ya misaada yamesema kizuizi hicho kinaweza kuwa uhalifu wa kivita na ni sawa na sera ya njaa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI