Header Ads Widget

MWENYEKITI WA CCM MBEYA MJINI APONGEZA UJENZI WA BARABARA ILOMBA - MACHINJIONI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini, Afrey Nsomba, amepongeza hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Ilomba - Machinjioni, ambao ni sehemu ya mradi wa TACTIC fungu la kwanza.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo akiwa ameambatana na kamati ya sisa wilaya na viongozi mbali mbali wa serikali, Nsomba alisema kuwa maendeleo yanayoonekana ni ishara ya dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuboresha miundombinu ya jiji la Mbeya na huduma kwa wananchi.

Barabara hiyo inajengwa na mkandarasi M/s Chongqing International Construction Corporation (CICO) kwa gharama ya shilingi bilioni 4.384,588,000. Mradi huo unatarajiwa kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa maeneo ya Ilomba, Machinjioni na viunga vyake.

Kwa upande wao Wananchi walieleza furaha yao juu ya maendeleo ya mradi huo, wakisema kuwa mara baada ya kukamilika, barabara hiyo itapunguza adha ya usafiri, hasa wakati wa mvua.

“Tumekuwa tukipata shida sana wakati wa mvua, magari yanashindwa kupita, lakini sasa tunaona matumaini mapya,” alisema mkazi mmoja wa Machinjioni.

Mradi wa TACTIC ni sehemu ya jitihada za serikali kuimarisha miundombinu ya barabara katika miji mbalimbali nchini, kwa lengo la kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI