Header Ads Widget

MKATABA WA UJENZI CHUO KIKUU CHA DODOMA TAWI LA NJOMBE WASAINIWA RASMI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Siku 365 ambazo ni sawa na Mwaka Mmoja zitatumika kujenga Chuo kikuu Cha Dodoma tawi la Njombe baada ya mkataba wa ujenzi kusainiwa rasmi Leo Mei 12 Mwaka huu.


Kwa mujibu wa Naibu mratibu wa mradi wa HEET toka Chuo kikuu Cha Dodoma Dokta Happiness Nnko amesema Kiasi Cha shilingi bilioni 17.17 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu sita ya Msingi katika Chuo hicho.



Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kikuu Cha Dodoma Profesa Rwekaza Mukandala amesema kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi kwenye vyuo vikuu Nchini Rais Samia aliamua kuongezwa kwa matawi ya vyuo Likiwemo tawi la Njombe.



Naye mratibu wa majenzi mradi wa HEET Kitaifa Mhandisi Hanington Kagiraki amemtaka mkandarasi wa mradi huo kutokwenda Kinyume na mkataba wake kwani hakuna Fedha za ongezeko nje ya mkataba.


Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema suala la Elimu kwa wakazi wa Njombe ni muhimu na wanahamasa kubwa ya kusomesha watoto wao.



Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni inayokwenda kutekeleza mradi huo ya Dimetoclasa Real hope Limited Bwana Dickson Mwipopo ameahidi kufikisha mitambo eneo la ujenzi ndani ya wiki hii na kuanza kazi mara Moja.



Nao wananchi mkoani Njombe akiwemo Frank Msuya na Justin Nusulupila Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe wamesema kwa miaka mingi Njombe ilikuwa inahitaji kupata Chuo kikuu kwa maslahi Mapana ya watoto na Taifa na sasa yametimia.



Chuo kikuu hicho hadi kukamilika kwake kitatumia shilingi bilioni 20.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI