Header Ads Widget

MBUNGE MUHONGO AMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA AKICHANGIA BAJETI YA ELIMU

Na Shomari Binda-Matukio Daima Media

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye jimbo lake kwenye sekta ya elimu.

Fedha hizo zimewezesha kuanzishwa na kujengwa kwa shule mpya za sekondari ikiwemo shule mpya ya Kumbukumbu ya Profesa David Massamba iliyofunguliwa hivi karibuni Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango.

Akianza kuchangia Wizara hiyo kwenye Bunge la 12 Mkutano wa 19 leo mei 12,2025 amesema jimbo hilo hawana budi kumshukuru Rais Dkt.Samia  kwa kile alichowafanyia.

Amesema licha ya kumshukuru mheshimiwa Rais wabunge wanapaswa kuipitisha bajeti ya Wizara ya Elimu kwa kuwa ndio roho ya nchi na inaleta mageuzi makubwa hususani katika mpango wa Dira ya Taifa ya 2025/2030.

Muhongo suala la ufundishaji,uelewa na ufaulu lazima viende pamoja na jimbo la Musoma Vijijini tayari imeshafanya mijadala ya elimu katika utekelezaji wake.

Amesema ushauri wake kutokana na Dira ya Maendeleo inayoanzia mwaka huu ni pamoja na ujenzi wa shule za magorofa kutokana na uhaba wa ardhi kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu huku ardhi ikibaki ile ile.

Mbunge huyo amesema ikifika juni mwaka huu idadi ya watanzania itafikia asilimia 70.55 hivyo ujenzi wa aina hiyo za shule ni muhimu kwa sasa.

Amesema elimu ni ajira na ndio yenye soko kubwa duniani hasa kupitia masomo ya sayansi hivyo lazima kuzalisha wasomi wengi zaidi.

"Mheshimiwa Waziri ujenzi wa shule lazima ubadilike na tujenge kwa kwenda juu kutokana na ufinyu wa a4dhi ambao tuko nao kwa sasa hapa nchini.

" Kwenye duala la ajira kupitia elimu kuna upungufu mkubwa duniani hasa eneo la teknolojia hivyo mtaala yetu iendane na kuwapata wanasayansi",amesema.

Amesema ili kuzipata ajira hizo sekondari zote zinapaswa kuwa na maabara pamoja na maktaba zitakazowezesha kupata wanasayansi wengi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI