Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ameupokea uongozi wa mgodi wa Shanta Gold kwaajili ya kufanya shughuli za uchimbaji.
Uongozi wa mgodi huo chini ya mkurugenzi wake mkuu Erick Zurin umepokelewa leo mei 23,2025 kwenye ofisi ya mkuu huyo wa mkoa.
Akizungumzia ujio wao wa kufika na kuja kuwekeza pmkoani Mara afisa uendeshaji wa mgodi huo Honest Mrema amesema wamevutiwa na hali ya usalama ya mkoa wa Mara na ndio iliyopelekea kuja kuwekeza.
Amesema licha ya hali nzuri ya usalama mazingira mazuri ya mkoa baada ya utafiti pia yamewafanya kuja kuwekeza.
Mrema amesema ndani ya miezi 18 watahakikisha wanajenga mgodi huo na wafanyakazi wengi watapewa wenyeji wa mkoa wa Mara.
Amesema .wamewekeza miaka 12 Tanzania na wakiwa mkoani Singida mahitaji mengi ya manunuzi wamekuwa wakiyafanya kwenye maeneo waliyowekeza.
Afisa huyo amesema mgodi huo pia umekuwa ukitoa fedha za CSR ambazo zimekuwa zikisaidia kwenye masuala ya kijamii ikiwemo kwenye elimu,afya maji na masuala mengine.
" Tunashukuru kufika na kupokelewa mkoa wa Mara sisi ni kampuni inayojishughulisha na uchimbaji na tumekuja kuwekeza mkoa wa Mara.
" Kwa namna ya mpokezi tuliyoyapata naamini tunakwenda kufanya kazi pamoja na mafanikio yake yataonekana ikiwa ni pamoja kusaidia jamii",amesema.
Akizungumza baada ya kuupokea uongozi wa mgodi huo,mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans ameikribisha kampuni hiyo na kuahidi kuipa ushirikiano wote.
Amesema mazingira ya uwekezaji ni mazuri na mkoa wa Mara ni sehemu sahihi na wamefanya uamuzi bora kuja kuwekeza.
Mkuu huyo wa mkoa amesema amefurahishwa na kusikia kipaumbele cha ajira kitakuwa vijana wa mkoa wa Mara na kusema anawaahidi kuwapa kila wanachokitarajia
" Niwakaribishe sana mkoa wa Mara kuja kufanya uwekezaji hapa ni sehemu nzuri na salama na ushirikiano wote mtaÄ·aouhitaji mtaupata",amesema.
0 Comments