Header Ads Widget

MBUNGE MATHAYO AFATILIA MALIPO YA WAFANYAKAZI KIWANDA CHA MUTEX


 Na Shomari Binda-Musoma 

SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda imeahidi kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha Mutex ili kupata haki yao baada ya kubinafsishwa.

Hayo yamesemwa leo mei 8 kwenye kipindi cha maswali na majibu katika Kikao cha 19 Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali dogo la nyongeza la mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.

Akijibu swali la mbunge huyo aliyetaka kujua ni lini wafanyakazi hao watalipwa malipo yao baada ya kukitumikia kiwanda hicho amesema serikali inatambua madai hayo na inaendelea na mipango ya kuhakikishwa wanalipwa.

Waziri huyo amempongeza mbunge huyo kwa ufatiliaji wake mara kwa mara kuhakikisha waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho wanalipwa madai yao.

Licha ya kuhakikisha wasnyakazi hao wanalipwa amesema serikali pia itahakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafatiliwa na kufufuliwa kwaajili ya uzalishaji pamoja na kuanzishwa kwa viwanda vipya.

" Mheshimiwa Mwenyekiti nitumie nafasi hii kwanza kumshukuru mheshimiwa mbunge Mathayo kuendelea kuwasemea waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hiki.

" Serikali inatambua madai haya na nimuhakikishie mbunge malipo haya yatalipwa na viwanda ambavyo vilibinafsishwa kuhakikisha vinafanya kazi na kuanzishwa viwanda vipya",amesema.

 Akizungumza na GMTV kuhuusiana na mbunge Vedastus Mathayo kuendelea kufatilia suala hilo bungeni,mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Mutex Shabani Kajala amemshukuru mbunge huyo kwa kufatilia malipo yao.

Amesema kama mwakilishi wao mara kadhaa amekuwa akiwasemea ili kufanikisha malipo yao na wanaamini serikali itatekeleza jambo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI