Na Matukio Daima App.
DODOMA.MBUNGE wa Mvumi, Livingstone Lusinde (CCM) 'Kibajaji' ameomba mambo manne kwa Wizara ya Kilimo ikiwemo kutoa elimu kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani kwani wananchi wa Jimbo la Mvumi wengi hawaujui.
Mengine aliyoyaomba ni uchimbaji wa visima ili mkulima aweze kulima na kufuga kwa urahisi, kutengenezwa kwa barabara ya Ndogole huku akimpongeza Waziri wa Wizara hiyo Hussein Bashe kwa kuweka mipango mizuri ya kupunguza bei ya sukari nchini.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo leo Mei 22,2025 bungeni, Lusinde amesema kunahitajika elimu kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani kwani wengi katika Jimbo la Mvumi hawaujui na hajui manufaa yake ni yapi.
"Mheshimiwa Waziri tunaomba katika stakabadhi ghalani kunahitajika elimu watu wakielewa watasimamia wenyewe ukiona watu wanakataa ni kwa sababu hawakifahamu hebu tufamisheni ili tuzungume kama watu wa Mtwara na jinsi ambavyo watu wanufaika.
Aidha ameiomba Wizara ya Kilimo kusaidia mashine za uchimbaji maji ziweze kufika katika Jimbo la Mvumi ili wananchi wawe kupata maji na kuwasaidia katika kilimo na ufugaji
"Kwenye BBT nikuombe wewe sio kazi yako pale Ndogole tutengeneze barabara pale kuna siku Rais atataka kwenda kule.Nikuombe Waziri utusaidie mmefikia wapi kuhusu wakala wa ugani,"amehoji Mbunge huyo.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuweza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa katika eneo la Manda na Mpwayungu.
"Nia ya Serikali ya awamu ya sita tumeiona katika kilimo Mkoa kama Dodoma hatutegemei kuingia katika kilimo cha umwagiliaji bila kujengewa mabwawa namna pekee ya kuingia katika soko ni kutengeneza mabwawa ambayo tutayatumia kufikia malengo yetu tunashukuru kwa kupatiwa mabwawa," amesema Kibajaji.
Pia alimshukuru Waziri Bashe kwa kusimamia vizuri suala la sukari kwani awali ikuwa ipo juu lakini wizara imepambana mpaka sasa hivi inauzwa Sh 2500 kutoka Sh 6000.
0 Comments