Header Ads Widget

KUNENGE ATAKA MATAKWA YA KISHERIA KWA WAFANYAKAZI YATEKELEZWE.

 





Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima App Kibaha


MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametoa wiki moja kwa waajiri kuhakikisha wanatekeleza matakwa ya kisheria juu ya stahiki za wafanyakazi.


Kunenge ameyasema hayo jana Mjini Kibaha wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.


Amesema kuwa waajiri wanapaswa kutekeleza matakwa ya kisheria ya juu ya haki za wafanyakazi ili waweze kufanya kazi vizuri bila ya malalamiko.


"Katika risala yenu kuna baadhi ya waajiri wanakiuka taratibu ikiwa ni pamoja na kutotoa mikataba ya kazi na stahiki nyingine jambo ambalo ni kinyume cha sheria,"amesema Kunenge.


Awali mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Pwani Susan Shesha amesema kuwa wanaishukuru serikali kuvutia wawekezaji ambapo imewezesha vijana wengi kupata ajira.


Shesha amesema kuwa changamoto iliyopo ni baadhi ya waajiri kutotoa mikataba ya ajira, fedha za matibabu, kutothibitishwa kazini, mapunjo ya mishahara, kuzuia uwepo wa vyama vya wafanyakazi sehemu za kazi, likizo na fedha za matibabu, vitisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI