Header Ads Widget

KENYA YAIOMBA TANZANIA KUMUACHIA MWANAHARAKATI BONIFACE MWANGI

 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imeitolea wito mamlaka nchini Tanzania kumuachilia mwanaharakati Boniface Mwangi anayekamatwa jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu.

Mwangi alikamatwa na watu wanaoshukiwa kuwa maafisa wa jeshi baada ya kusafiri kutazama kesi ya uhaini ya kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu siku ya Jumatatu. Bado hajulikani alipo.

Taarifa, wizara hiyo kwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Kenya imesema "licha ya maombi kadhaa, maafisa wa Serikali ya Kenya wamenyimwa ufikiaji wa kibalozi na habari kumhusu Bw Mwangi."

"Wizara pia ina wasiwasi juu ya afya yake, ustawi wa jumla na kukosekana kwa habari kuhusu kuzuiliwa kwake," ilisema.

Kenya imetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua ya "haraka na bila kuchelewa" ili kuwezesha ufikiwaji wa kibalozi au kuachiliwa kwa Mwangi, kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimataifa kidiplomasia.

Kenya na Tanzania ni nchi wanachama wa Mkataba wa Vienna wa 1963 wa Mahusiano ya Kibalozi, ambao unasema kwamba maafisa wa kibalozi watakuwa uhuru wa kuwasiliana na kuwafikia raia wa nchi iliyowatuma kuweza kuwafikia.

Aidha maafisa wa kibalozi wana haki ya kumtembelea raia wa taifa alikotoka wakati anapokuwa gerezani au kizuizini kuzungumza na kuwasiliana naye, na kupanga uwakilishi wake wa kisheria.

Mke wa mwanaharakati huyo wa Kenya, mwandishi wa habari Njeri Mwangi, Jumatano alisema alitembelea Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi ambapo maafisa walimwambia hawakuwa na habari kuhusu mumewe.

"Mara ya mwisho nilizungumza na Boniface Jumatatu alasiri. Mamlaka ya Tanzania inasema wamemfukuza lakini kwanini hakuna mawasiliano? Bonnie yuko wapi?" aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi.

"Turudishieni Boniface, amejeruhiwa au amekufa. Imekuwa chungu sana kwa familia yangu na sio haki au sawa kile wanachomfanyia."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI