Header Ads Widget

JAJI AFUNGWA JELA MIAKA 6 KWA KUMFANYA MFANYAKAZI WA NYUMBANI MTUMWA

 

Lydia Mugambe aliobainika kutumia vibaya nafasi yake ya madaraka kumtumia msichana huyo kama mtumwa

Jaji wa Umoja wa Mataifa amehukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi minne jela kwa kumlazimisha mwanamke kufanya kazi kama mtumwa wa nyumbani.

Lydia Mugambe, 50, alikuwa akisomea Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Oxford wakati polisi walipogundua kuwa alikuwa na msichana mdogo wa Kiganda nyumbani kwake akifanya kazi isiyolipwa kama mjakazi na yaya.

Mugambe, ambaye pia ni jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda, alihukumiwa kufungwa katika Mahakama ya Oxford siku ya Ijumaa baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya utumwa wa kisasa mwezi Machi.

Katika hukumu hiyo, Jaji David Foxton alimwambia mshtakiwa "hakuonyesha kujutia kabisa" kwa kitendo chake na alikuwa anatazamia "kumlaumu" muathiriwa kwa kile kilichotokea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI