NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kukubali kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi nane katika mikoa mbalimbali nchini huku majimbo 12 yakibadilishwa majina.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amesema Katika mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Mbeya mjini limegawanywa na kuanzishwa jipya la Uyole
Katika mkoa wa Dodoma, limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Dodoma mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba
Mkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo jipya la Bariadi mjini ambapo jimbo la Bariadi limegawanywa.
Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili ambayo ni Katoro na Chato Kusini yakigawanywa majimbo ya Busanda na Chato.
Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa jipya la Itwangi.
Katika Mkoa wa Dar es salaam Majimbo mawili yamegawanywa na kuanzishwa majimbo mapya mawili ambapo Ukonga limegawanywa na kuanzishwa jipya la kivule, na jimbo la mbagala limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Chamazi.
0 Comments