Header Ads Widget

MPANGO JUMUISHI NA HARAKISHI KUPUNGUZA UDUMAVU WAZINDULIWA NJOMBE

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali ya mkoa wa Njombe imepanga kupambana na udumavu kwa  watoto Toka Asilimia 40 ya sasa Hadi Asilimia 25 ifikapo Mwaka 2030  kwa Zaidi ya watoto laki Moja wa mkoa mzima.

Katika uzinduzi wa mpango jumuishi na harakishi wa kupunguza udumavu na kuzindua mradi wa Lishe ya mwanao mkoa wa Njombe katika Kijiji Cha Usita kata ya Ulembwe wilayani Wanging'ombe mkuu wa mkoa Antony Mtaka amesema ni lazima kukemewa kwa mambo ya hovyo yanayofanywa na vijana kuendekeza usasa na kusahau malezi ya watoto.

Mwakilishi wa Shirika la watoto Duniani UNICEF Nchini Tanzania Elke Wisch amesema Shirika Hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto za Lishe kwa watoto hususani katika mkoa wa Njombe ambao kwa sasa ni wa pili Kitaifa kwa udumavu.


Naye Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dokta Juma Mfanga amesema mpango huo umezinduliwa ukiwa na lengo la kuwapa mwanga wadau wote juu ya Nini kilichopo kwenye Lishe pindi wanapotaka  kuunga mkono.



Baadhi ya wananchi mkoani Njombe wamesema wapo Tayari kutekeleza mpango huo licha ya Changamoto za mapambano ya Uchumi yanayowakabili.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule mbalimbali za Msingi wilayani Wanging'ombe Wamesema changamoto ya udumavu imewafanya kulima mbogamboga katika maeneo ya shule pamoja na matunda Ambayo yanawasaidia katika Lishe.



Kauli mbiu ya kampeni ya Lishe mkoani Njombe ambayo imekuwa ni kauli mbiu ya Kitaifa ni''Kujaza tumbo sio Lishe,Jali unachomlisha''.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI