Header Ads Widget

ENG. KUNDO AFIKA KATA YA SAPIWI KUWASILISHA ILANI YA CCM.

 Mbunge wa Jimbo a Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew akipokelewa kwa shangwe na Wananchi wa Kata ya Sapiwi kwenye mkutano wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.



MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amewasili kata ya Sapiwi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalumu wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Katika Mkutano huo, Mbunge huyo amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo Jimboni humo na kwamba wananchi wamenufaika na miradi hiyo kwenye sekta za Maji, Umeme, Afya, Barabara, Elimu na Miundombinu mingine.



Akiwa kwenye kata hiyo, Mhandisi Kundo atagawa vifaa vya michezo kwenye Matawi ya Sapiwi, Nyamikoma, Mwandama, Igegu na Igegu Magharibi  ambapo kila tawil litapewa mipira minne na jezi moja ya jezi wakati huo kata ya Sapiwi ikipatiwa Mipira mitatu na jezi pea moja ili kuunga Mkono jitihada za Rais Dk.Samia kwenye sekta ya michezo.



Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, atagawa pampu tano za Maji zenye thamani ya shilingi Mil. 17.5 ili kuwasogezea wananchi huduma ya Maji huku akiwashukuru wananchi kwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Mwisho.
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI