Na Mwandishi Wetu, Kalambo
MRADI wa Kilimo na Lishe Tanzania (NOURISH -Tanzania), umelenga kuwafikia wakulima 168,000 katika mikoa mitano nchini kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu kilimo cha tija pia kuleta mapinduzi kwenye sekta hiyo.
Ofisa wa Mradi wa NOURISH, Fikilio Gambi amesema tangu mradi huo uanze mwaka jana umewafikia wakulima 13,556 katika mikoa ya Rukwa na Songwe .
Alisema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo Norway (Norad) na kutekelezwa na wadau wa maendeleo SNV pamoja na Farm Africa kupitia washirika wake RECODA na MIICO.
Gambi alisema mikoa mitano itakazonufaika na elimu hiyo ni pamija na Dodoma, Manyara, Rukwa, Singida na Songwe.
“Mradi wa NOURISH wilayani Kalambo umefanikiwa kuelimisha juu ya wananchi jinsi ya kuanzisha mashamba darasa 195 kwa mazao ya mtama,maharagwe na alizeti pia kuwaunganisha wakulima na kampuni za pembejeo za kilimo " anasema Gambi.
Anaongeza kuwa mradi ho umeanzisha 130 vikundi vya kilimo vimepewa pembejeo za kilimo kwenye mashamba darasa kwa kugawiwa kilogramu za mbolea kilogramu 2,458, mbegu bora kilo 760,viatilifu lita 130 na viuakuvu kilo 65.
Mwisho
0 Comments