Na. Stanley Brayton,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Dkt. Ashatu kijaji amezindua mnada wa Mpakani Kileo uliopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambao unatarajia utaongeza masoko ya mifugo.
Mnada huo ambao utakuwa fursa ya kimkakati kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi una uzio wa mzunguko wa mita 500, kipakilio, mazizi, choo pamoja na miundombinu ya maji kwa ajili ya wafugaji na wafanyabiashara Mkoani Kilimanjaro umegharimu Sh.milioni 208.924 hadi kukamilika.
“Mnada huu una uwezo wa kupokea ng’ombe 500 na mbuzi na kondoo 3000 kwa mara moja na hivyo ni imani yangu kuwa uwekezaji huu utaleta tija na miundombinu iliyojengwa itatunzwa na kulindwa," alisema Dkt. Kijaji.
Alisema ujenzi wa mnada huo ni muendelezo wa utekelezaji wa dhamira njema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan kwa wafugaji na wadau wa mifugo nchini katika kupanua masoko ya mifugo ndani na nje ya nchi.
Alisema hadi sasa minada ya mifugo 51 yenye thamani ya Sh. Bilioni 17.5 imejengwa na kukarabatiwa hapa nchini ambayo imewezesha ongezeko la biashara ya mifugo nchini.
Dk.Kijaji kutokana na uwepo wa minada, mifugo iliyouzwa katika minada hiyo imeongezeka kutoka Sh. Trilioni 1.5 2021/22 hadi kufikia Sh. Trilioni 3.7 mwaka 2024/25.
Aidha, Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi amewataka wafanyabiashara ya mifugo hususani wanaosafirisha mifugo kwenda nje ya nchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi katika kufanya biashara hiyo.
Aliongeza kuwa kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaaminifu ambao kwa makusudi hufanya biashara kinyume na taratib, na hutumika na wafanyabiashara wa nchi jirani kununua na kutorosha mifugo kwa siri kwa kutumia vipenyo visivyo rasmi kwenda nchi jirani.
Alisema wakati mwingine wafanyabiashara kutoka nchi jirani huingia na kwenda moja kwa moja katika minada ya awali kwa kuwatumia wenyeji kununua mifugo hiyo na kuisafirisha kinyume na taratibu kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

0 Comments