Header Ads Widget

DIWANI AKEMEA USHIRIKINA KWENYE MIRADI ANAYOSIMAMIA


Baadhi ya wananchi wa kata ya Kitongoni na maeneo jirani ya kata hiyo katika manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo Himidi Omari.


Na Fadhili Abdallah, Kigoma


DIWANI wa kata ya Kitongoni Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji Himidi Omari amesema kuwa ilani ya uchaguzi ya CCM yam waka 2020 imetekelezwa kikamilifu kwenye kata hiyo huku akikemea watu wanaofanya vitendo vya kishirikina kwenye miradi anayoisimamia ili kukwamisha miradi hiyo.


Himidi amesema hayo akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kabondo Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji na kubainisha kuwa kata hiyo na halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo na idadi kubwa ya miradi imetekelezwa na kutoa huduma kwa wananchi.


Diwani huyo amesema kuwa katika miaka mitano ambayo amekuwa diwani katika kata hiyo ameweza kutekeleza mradi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa zahanati, madarasa 12 ya sekondari Kitongoni, kupatikana fedha za kujenga matundu 17 ya vyoo na sasa zimepatikana fedha  kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za walimu sambamba na kuimarishwa kwa barabara.


Amesema kuwa wakati akifanya kazi kubwa ya kupigania miradi amekumbana na tabia ya watu wasiopenda maendeleo ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya kishirikina kwenye miradi ikiwemo mradi wa soko la jioni Ujiji ambapo alipambana ikiwemo kutoa fedha yake ya mfukoni ili  soko hilo  liweze kufanya kazi hadi usiku ambao vitendo vya kuvuja vyungu na nazi vimetawala kwenye mradi huo ili kukwamisha mradi usifanye kazi.


Awali katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kigoma Ujiji , Haruna Kambiro akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa chama kimeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na madiwani wa chama hicho ambao kwa sasa ndiyo wanaoendesha halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo miradi mingi imetekelezwa ikiwemo iliyotumia mapato ya ndani.


Kambiro amesema kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo kunatokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya madiwani hao, serikali na chama tawala ambapo kwa utatu wao umewezesha kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo kwenda kwa wananchi.


Kwa upande wake Diwani wa viti maalum, Hellen Beji amesema kuwa kwa miaka mitano ambayo madiwani walifanya kazi kwa pamoja wameweza kuongeza makusanyo ya ndani kutoka milioni 140 waliopoingia na kufikia milioni 400 kwa mwezi  ambapo miradi mingi imetekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani.


Mwisho.


Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Kigoma Mjini Haruna Kambiro akizungumza katika mkutano ulioitishwa na Diwani wa kata ya Kitongoni Ujiji mjini Kigoma.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI