Header Ads Widget

CRDB BENK MUSOMA KUIPA USHIRIKIANO TAASISI YA NASIMAMA NA MAMA

Na Shomari Binda-Musoma 

BENKI ya CRDB tawi la Musoma imeahidi kuipa ushirikiano taasisi ya "Nasimama na Mama" baada ya kufika kujitambulisha kwao.

Akizungumza na Matukio Daima ofisini kwake meneja wa benki hiyo tawi la Musoma Jerome Mwenda amesema ameupokea uongozi wa taasisi hiyo na kufanya nao mazungumzo na kuahidi kushirikiana nao.

Amesema moja ya malengo ya taasisi hiyo ni kuifikia jamii na kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mambo ya ujasiliamali na wao kama wadau hawana budi kushirikiana nao.

Mwenda amesema kwenye eneo la ujasiliamali kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambayo taasisi hiyo inakwenda kuitolea elimu kwa jamii wanahusika nayo.


Amesema wanapokwenda kutoa elimu hiyo kwa kushirikiana na halmashari wapo tayari kushirikiana nao kuifikia jamii kwa kutoa elimu.

Jambo lingine ambalo amesema meneja huyo na kuahidi kuipa ushirikiano taasisi ya " Nasimama na Mama" ni kwenda kusemea mazuri yanayofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.

" Wamekuja kunitembelea hapa viongozi wa taasisi ya "Nasimama na Mama"na tumefanya nao mazungumzo na tupo tayari kushirikiana nao.

" Wanakwenda kuifikia jamii kwenye masuala ya ujasiliamali na sisi ni wadau hivyo tutakwenda kushirikiana kwa kuwapa elimu",amesema.

Taasisi ya Nasimama na Mama iliyopo manispaa ya Musoma kupitia Mwenyekiti wake Ibrahim Assey imekuwa ikipita ofisi mbalimbali ikiwemo ya mkuu wa mkoa wa Mara kwaajili ya kujitambulisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI