Header Ads Widget

ASIA ABDALLAH AHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Asia Abdallah, ambaye pia aliwahi kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Chemba kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.

Asia ametoa wito huo wakati wa zoezi lake wilayani humo, iliyolenga kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uboreshaji wa daftari hilo, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

 “Leo nimebahatika kutembelea Wilaya hii ya Chemba na nimekutana na makundi mbalimbali, wakiwemo wajasiriamali, akinamama, vijana wa bodaboda na wafanyabiashara. 

Wengi wao wamehamasika na tayari wamejiandikisha, na kwa wale wachache ambao hawakufanya hivyo, tumewapa elimu na kuwaelekeza jinsi ya kujiandikisha na kupata vitambulisho vyao vya kupiga kura,” amesema Asia.

Ameongeza kuwa mbali na kujiandikisha, wananchi wanapaswa pia kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi, kwani hatua hizo mbili ni tofauti na kila moja ina umuhimu wake katika kuhakikisha haki ya kidemokrasia inatimia.

“Kupiga kura kunahitaji watu. Kujiandikisha ni hatua ya kwanza, lakini kushiriki uchaguzi ni hatua nyingine muhimu. 

Hii ni haki ya kila Mtanzania ya kuchagua viongozi wanaowataka. Ukizingatia kuwa kesho ni siku ya mwisho ya zoezi hili, niwaombe wananchi kutumia nafasi hii muhimu kabla haijapita,” amesisitiza.

Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, awamu ya pili, linatarajiwa kufikia kikomo Mei 22, 2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI