Header Ads Widget

ZANZIBAR AFYA WEEK 2025 YATAMBULISHWA DAR, MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA ZANZIBAR



Na Andrew Chale, Matukio Daima App Dar.

WAZIRI wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema takribani wagonjwa 200 kila mwezi kutoka Zanzibar huenda Tanzania Bara kwa ajili ya kupata mtibabu ya kibingwa na bobezi hali ambayo inaendelea kudumisha Muungano.

Waziri Mazrui amesema hayo April 11,2025 Jijini Dar Es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Afya Zanzibar, (Zanzibar Afya Week 2025) Unguja na Pemba yenye kauli mbiu 'Tuanze safari ya Mabadiliko kwenye sekta ya Afya' inatarajiwa kuanza Mei 4 hadi Mei 10, 2025 Zanzibar.

Katika mkutano huo uliofanyika hoteli ya Johari Rotana, umehusisha pia wadau mbali mbali wa sekta ya Afya kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, 

Ambapo amesema kuwa, ushirikiano huo wa tiba unafanya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutumia kiasi cha si chini ya shilingi milioni 400 kugharamia matibabu ya wagonjwa hao zaidi ya 200 kwa mwezi.


"Naomba niwe mkweli Zanzibar tuna Madaktari 134 na kati yao Wabobezi ni wanne tu, hivyo kufanya wagonjwa wetu kuja Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Upanga, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mlogazila kwa ajili ya kuja kupata matibabu.

"Si chini ya Sh milioni 400 zinalipwa na SMZ kwa ajili ya watu hao kupata huduma na hiyo ni kutokana na mashirikiano mazuri kati ya Serikali hizi mbili". Amesema Mazrui

Amesema katika wiki hiyo ya Afya wamelenga kuboresha Sekta ya Afya, tiba utalii kwani kwa mwezi watalii 200 hufika Visiwani humo kwa ajili ya kupata huduma za tiba mbali mbali na hulipia fedha nyingi hivyo zitasaidia kukuza pato la Taifa na kuongeza ajira kwa vijana.

Aidha, Mazrui amesema maadhimisho hayo yamelenga kuvutia uwekezaji watakao kuja kuimarisha miundombinu ya Afya pamoja na kuboresha mazingira ya kazi yatakayoboresha afya ya akili kwa watumishi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mangere Miraji amesema katika wiki hiyo watakuwa na mambo manne ikiwemo kuongeza uelewa wa afya kwa jamii , kutambua mchango wa wadau mbali mbali kupitia sekta ya Afya, kujuza utalii wa tiba na kuongeza mapato ya tiba na kuhamasisha ushiriki na matumizi ya tenkolojia katika sekta ya afya.

" Utalii wa afya kwa kushirikiana na wadau wa Afya kutoka Dar es Salaam utarahisha mahusiono katika kuboresha sekta ya afya ambapo hii itasaidia kuwafikia makumdi mbalimbali yenye changamoto za maradhi,"


Naye, Mganga Mkuu mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Mohamed Mang'una amesema wataendelea kushirikiana kwa ukaribu na sekta binafsi ili kudumisha utalii wa afya bara na visiwani ilikuhakikisha malengo mahususi yanatimilika.

"Hii itasaidia kuunganisha sekta binafsi za afya na sekta za umma kwa kufanya utalii wa afya utakaoweza kukuza pato la Taifa na kutoa ajira kwa vijana " amesema Dkt. Mang'una


Mkurungezi wa Jiji la Dar es salaam, Elihuruma Mabelya amesema uzinduzi huo unakwenda kutoa msingi katika eneo hilo na mkoa uko tayari kushiriki mpango huo kupitia vikao vya ndani ili kuleta mabadaliko makubwa katika sekta ya afya.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuwa alama kubwa kwa Zanzibar kwani yatahusisha wadau mbalimbali watakaofika pamoja na huduma za tiba za kibingwa na bobezi.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI