Header Ads Widget

WATU 79 WAFARIKI BAADA YA KLABU YA BURUDANI KUPOROMOKA HUKO JAMHURI YA DOMINICAN

 

Watu wanalia na kukumbatiana karibu na klabuya burudani ya Jet Set huko Santo Domingo


Maafisa wa uokozi katika Jamhuri ya Dominican wanasema watu takriban themanini wamefariki dunia na 150 kujeruhiwa baada ya paa la ukumbi wa burudani kuanguka wakati wa tamasha la msanii Rubby Perez.

Msanii huyo ni miongoni mwa hao waliofariki dunia.

Maafisa hao wa uokozi wanawatafuta manusura katika ukumbi huo ulioko mji mkuu Santo Domingo uliojengwa miaka ya sabini iliyopita.

Mkurugenzi wa Kituo cha Operesheni za Dharura (COE), Juan Manuel Méndez, alisema ana matumaini kwamba wengi wa waliozikwa chini ya paa lililoporomoka bado wako hai.

Jet Set ni klabu ya usiku maarufu huko Santo Domingo ambayo huandaa mara kwa mara matamasha ya muziki wa dansi Jumatatu jioni.

Wanasiasa, wanamichezo na watu wengine mashuhuri walihudhuria.

Pia miongoni mwa wahasiriwa ni Nelsy Cruz, gavana wa jimbo la Monte Cristi, Rais Luis Abinader alisema.

Alikuwa dada wa mchezaji wa zamani wa besiboli Nelson Cruz, mchezaji nyota wa Ligi Kuu mara saba.

Dotel alianza kuchezea New York Mets mnamo 1999 na alichezea timu zikiwemo Houston Astros, Oakland A's, New York Yankees, Chicago White Sox na Detroit Tigers hadi 2013.

Picha za video zilizochukuliwa ndani ya klabu zinaonyesha watu wameketi kwenye meza mbele ya jukwaa na wengine wakicheza kwa muziki nyuma huku Rubby Pérez akiimba.

Katika rekodi tofauti ya simu ya mkononi iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamume aliyesimama karibu na jukwaa anasikika akisema "kitu kimeanguka kutoka kwenye dari", huku kidole chake kikionekana kikielekezea paa.

Katika picha hiyo, mwimbaji Rubby Pérez, pia anaonekana kutazama eneo lililoonyeshwa na mtu huyo.

Hazikupita sekunde 30, kelele zinasikika na rekodi hiyo kuwa giza huku mwanamke akisikika akipiga kelele "Baba, umepatwa na nini?".

Rais Abinader ametoa rambirambi zake kwa familia zilizoathirika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI