Header Ads Widget

UKRAINE YAKAMATA WACHINA WAWILI WANAOPIGANIA URUSI- ZELENSKY



Rais wa Ukraine Zelensky alisema kuwa inawasiliana na Beijing ili kupata majibu

 Wanajeshi wa Ukraine wamewakamata raia wawili wa China waliokuwa wakipigana upande wa jeshi la Urusi katika mkoa wa Donetsk, amesema Rais Volodymyr Zelensky.

Rais wa Ukraine ameeleza kuwa idadi ya raia wa China walio katika jeshi la urusi ni ‘’wengi zaidi’’.

Waziri wa masuala ya kigeni wa Ukraine Andrii Sybiha ametamaushwa na uwepo wa vikosi vya China vinavyopigana Ukraine akishauku msimamo wa China wa kutaka amani nchini humu .

Aidha ameongezea kuwa ujumbe wa China nchini Kyuv umewajibishwa kuelezea ni kwanini vikosi vyake vinapigana na adui wa Ukraine.

Ni tangazo la kwanza rasmi la Ukraine kuhusisha China kupatia Urusi vikosi vyake vya kijeshi.

Hata hivyo, hakuna jibu lolote limetolewa kutoka sasa na upande wa Urusi wala Beijing.

Korea Kaskazini imetuma maelfu ya wanajeshi kusaidia juhudi za vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, kwa mujibu wa Kyiv na maafisa wa Magharibi.

Wakati Beijing na Moscow ni washirika wa karibu wa kisiasa na kiuchumi, China imejaribu kujionyesha kama upande usioegemea upande wowote katika mzozo huo na mara kwa mara imekana kuipatia Urusi zana za kijeshi.

Moja ya faida kuu za Urusi katika vita ni idadi kubwa ya vikosi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alizindua uvamizi kamili dhidi ya Ukraine mnamo 2022, na Moscow kwa sasa inadhibiti karibu asilimia 20% ya ardhi ya Ukraine, haswa mashariki.

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine ziliendelea Jumanne usiku na kujeruhi watu 14 katika jiji la kati la Ukraine la Dnipro, na mengine mawili huko Kharkiv, kaskazini-mashariki, maafisa wa eneo hilo walisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI