Katibu Tawala wa wilaya Kigoma Mganwa Nzota
Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
Watoto wawili wakazi wa eneo la Kibirizi manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mvua walipokuwa wakicheza kwenye mvua karibu na nyumbani kwao Jumamosi hii ya pasaka.
Katibu Tawala wa wilaya Kigoma, Mganwa Nzota alisema hayo akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya Kigoma,Rashidi Chuachua aliyekuwa akikutana na wananchi wa eneo la Katubuka walioathirina na mvua hiyo ambao nyumba zao zimevamiwa na maji na kulazimika kuyahama makazi yao.
Nzota alisema kuwa katika tukio la kusombwa na maji alisema kuwa watoto hao walikuwa wakioga kwenye mtaro jirani na nyumba yao wakati mvua ikinyesha na hivyo kusombwa na maji hayo ya mvua ambapo maiti za watoto hao ziliokotwa eneo la bandari ndogo ya Kibirizi.
Mazishi ya watoto hao yamefanyika jana na leo katika maeneo hayo ya Kibirizi ambapo Mkuu wa wilaya Kigoma,Rashid Chuachua ametoa wito kwa wazazi kuchukua hatua za tahadhari kwa watoto wao wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha katika wilaya hiyo.
Mwisho.
0 Comments