Na Fadhili Abdallah
Wachakataji wanawake wa mazao ya uvuvi kutoka kata za Mwakizega na Ilagala katika halmashauri ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma wameanza kupatiwa mafunzo ya kuongeza thamani mazao ya uvuvi na uendeshaji biashara ili kuzifanya shughuli zao kuwa na tija kubwa.
Mratibu wa mpango wa kuwajengea uwezo wanawake kuhusu uchakataji wa mazao ya uvuvi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Muyobozi Environment Conservation,Kessi Yakuti alisema hayo wakati wa uzinduzi wa program hiyo ya miezi mitatu iliyofanyika Mwalo wa kijiji cha Muyobozi wilaya ya Uvinza mkoa Kigoma.
Mratibu wa mpango wa kuwajengea uwezo wanawake kuhusu uchakataji wa mazao ya uvuvi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Muyobozi Environment Conservation,Kessi Yakuti
Yakuti alisema kuwa katika mpango huo unaofadhiliwa na Shirika la Action Fund For Africa, wanatarajia kutoa elimu kwa viongozi 33 kutoka vikundi 11 vya wanawake wanaojishughulisha na uchakataji wa mazao ya uvuvi ambao baada yaa mafunzo hayo wanawake hao viongozi watatumia nafasi zao kuwafikishia elimu wachakataji wenzao 500 wanaofanya kazi pamoja kwenye vikundi vyao.
Mratibu huyo alisema kuwa mradi huo unakuja kukiwa na changamoto kubwa iliyopo ambayo inasababisha kupotea na kuharibika kwa mazao ya uvuvi baada ya kuvuliwa hivyo mafunzo hayo yatawezesha uchakataji wenye tija ambao hautapoteza mazao mengi ya uvuvi lakini pia itasaidia biashara ya mazao ya uvuvi kuzingatia ubora na kuwa na tija.
Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya Uvinza, Christopher MutabaziKwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya Uvinza, Christopher Mutabazi alisema kuwa kuongezwa thamani kwa mazao ya uvuvi ndiyo mpango unaoleta tija kubwa kwenye masuala ya biashara na kufanya biashara hiyo kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa lakini pia kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.
Mwisho.
0 Comments